January 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Rais Kikwete azindua ujenzi wa bandari ya Bagamoyo

Spread the love

UJENZI wa bandari inayotarajiwa kuwa ya kwanza kwa ukubwa kuliko zote katika kanda ya Afrika Mashariki umeanza mjini Bagamoyo mkoa wa Pwani.

Bandari hiyo inayojengwa maeneo ya Mbegani mjini Bagamoyo, umezinduliwa rasmi leo na Rais Jakaya Kikwete.

Bandari hiyo itakuwa na uwezo wa kupokea shehena milioni 20 kila mwaka, idadi ambayo ni mara mbili zaidi ya bandari ya Dar es Saalam.

Mradi huo utagharimu takriban dola bilioni 11, huku ufadhili mkubwa wa kiasi hicho ukitoka nchini China.

Serikali ya Tanzania inasema kuwa mradi huo utaiwezesha kushindana na Kenya katika biashara za kikanda na kimataifa.

Bandari hiyo inatarajiwa kutoa ushindani mkali kwa bandari iliyo mjini Mombasa katika taifa jirani la Kenya.

Mji wa Bagamoyo umo kilomita 75 kaskazini mwa Dar es Salaam na ndilo eneo anamotoka Rais Jakaya Kikwete anayemaliza madaraka yake baada ya uchaguzi wa urais Oktoba 25.

Bagamoyo ulikuwa ndio mji mkuu wa awali wa kikoloni chini ya Wajerumani na ulikuwa kituo kikuu katika biashara ya utumwa. Watumwa waliwekwa katika mji huo kwa muda kabla ya kusafirishwa hadi soko kuu katika kisiwa cha Zanzibar.

error: Content is protected !!