
Rais Jakaya Kikwete akitoa salamu zake za mwezi mtukufu wa Ramadhani kwa baadhi ya watoto yatima aliowaalika Ikulu
VIONGOZI wa nchi wanatakiwa kuwa mfano bora katika kuisaidia jamii kwa namna yoyote ile hususani kwa watu waishio katika mazingira magumu na wasiojiweza ili wawe mfano wa kuigwa. Anaandika Sarafina Lidwino … (endelea).
Kwa kuzingatia hilo, Rais Jakaya Kikwete ametoa misaada ya vyakula vyenye thamani ya sh. Milioni saba katika vituo tofauti 15 vyenye watu wenye makundi maalum ili nao waweze kuifurahia sikukuu hii ya Eid el Fitri.
Akikabidhi misaada hiyo kwa niaba ya Kikwete, katika mahabusu ya watoto iliyopo Upanga Jijini Dar es Salaam, Kamishna msaidizi wa Wizara ya Afya na Ustawi wa jamii, Beatrice Fungamo, amesema misaada hiyo iliyotolewa ilikuwa na lengo la kuwafanya watoto hao nao waifurahie sikukuu hii.
Fungamo alibainisha misaada hiyo iliyotolewa kuwa ni, mafuta ya kupikia, mafuta na mchele ambapo vilipelekwa katika vituo 7 vya hapa Dar es Salaam, viwili vya Zanzibar, pamoja na mikoa ya Mbeya, Arusha , Morogoro ,Tanga, na Kilimanjaro.
Akitoa shukurani mmoja kati ya walezi wa vituo hivyo, wakati akipokea msaada huo, Shabani Mohamed wa kituo cha watoto cha Daral Argum Kilichopotemeke alsma, “tunamshukuru Rais Kikwete kwa kutoa msaada huu ambao utawza kuwasaidia watu wasijiweza.
More Stories
Barrick ilivyoshiriki katika kuadhimisha Siku ya Canada
PURA yaanzisha kanzidata
Branch kufikisha mikopo ya haraka kwa mamilioni ya Watanzania