January 23, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Rais Kikwete apewa somo

Spread the love

RAIS Jakaya Kikwete ameshauriwa kuingilia kati swala la mgogoro wa kisiasa uliyojitokeza visiwani Zanzibar kutokana na kufutwa kwa matokeo ya uchaguzi Mkuu wa Urais visiwani hapo. Anaandika Dany Tibason, Dodoma … (endelea).

Mbali na kumtaka rais kuingilia mgogoro huo imeelezwa kuwa, taasisi na idara nyingi za serikali kwa sasa hazina fedha za kuendesha miradi mbalimbali ya kiuchumi kwa kuwa fedha nyingi zilitumika kipindi cha uchaguzi, na hivyo, kipidi hiki ni vyema kikatumika kwa ajili ya kuimarisha uchumi wa chi.

Akiongea na MwanaHALISI Online mapema jana, Katibu wa Chama Cha Wafanyakazi Kanda ya Kati, Ramadhani Mwenda amesema kama Rais Kikwete hataingilia kati mpasuko wa kisiasa visiwani Zanzibar, atakuwa hajamtendea haki Raisi mteule, Dk. John Magufuli.

“Unajua serikali ilitumia fedha nyingi sana wakati wa uchaguzi kiasi kwamba kwa muda huu idara nyingi haziwezi kufanya kazi ipaswavyo kwa sababu ya upugungufu wa fedha. Hivyo, ni vyema swala hili likathibitiwa mapema ili watanzania watulie na kufanya shughuli za kuimarisha uchumi wa nchi,” alieleza.

Aidha, aliongeza kuwa swala la mpasuko wa kisiasi Zanzibar haliwezi kudhibitiwa na jeshi la Polisi peke yake, bali ni swala linalohitaji mawazo ya kidiplomasia zaidi.

“Sidhani, na wala sina imani kwamba nguvu ya Jeshi inaweza kumaliza mgogoro wa Zanzibar kwani chanzo chake ni siasa, hivyo hata kulimalizaswala hilo kunahitaji mawazo imara ya kisiasa pia,” aliongeza.

Aliongeza kuwa akili za wafanyakazi wengi hivi sasa nchini zimehamia Zanzibar kwa kiasi kwamba wanashindwa kujikita katika uzakishaji wa uchumi, hivyo Rais Kikwete anapasika kuhakikisha kwamba swala hilo linaisha kabla hajamkabidhi nchi Dk. Magukuli.

“Itakuwa heshima kubwa sana kama Rais Kikwete atamaliza mgogoro wa Zanzibar na kumkabidhi Dk. Magufuli nchi yenye utulivu, na yenye wananchi waliyotayari kufanya kazi,” aliongeza.

error: Content is protected !!