January 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Rais Kikwete anywea, Mahakama ya Kadhi yaota mbawa

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete akitafakari jambo

Spread the love

MAHAKAMA ya Kadhi imeota mbawa. Muswaada uliopangwa kuwasilishwa bungeni leo, tayari umeondolewa na mjadala wake kufungwa. Anaandika Saed Kubenea… (endelea).

Kuondolewa kwa Muswaada wa Mahakama ya Kadhi, kumefuatia shinikizo la viongozi wa madhehebu ya Kikiristo, “wanaoungwa mkono chini kwa chini na Chama Cha Mapinduzi (CCM),” anaeleza mtoa taarifa ndani ya Baraza la Mawaziri.

Mkutano wa Baraza la Mawaziri uliodhinisha kuondolewa kwa muswaada ulifanyika mjini Dodoma jana, chini ya mwenyekiti wake, Dk. Jakaya Mrisho Kikwete.

Taarifa kutoka ndani ya kikao cha baraza la mawaziri zinasema, kuondolewa kwa muswada kumetokana na hofu kuwa “kuundwa kwa Mahakama ya Kadhi, kutawakasirisha Wakristo.”

“Muswaada huu umepigwa chini kutokana na shinikizo la waamini wa madhehebu ya Kikristo. Hii ni kwa sababu, CCM tokea awali walikuwa wanapinga kuwapo kwa mahakama hii. Lakini walifanya hivyo kimyakimya kwa kuhofia hasira za Waislamu,” anaeleza mtoa taarifa.

Kwa mujibu wa andishi kutoka ndani ya chama hicho la 27 Januari 2015, lililobeba kichwa cha maneno, “taarifa muhimu za magazeti,” chama hicho kinasema msimamo wa “madhehebu ya kikirsto unapaswa kuungwa mkono na jumuiya nyingine za kidini.”

Andishi linasema, “Lakini CCM isijiingize waziwazi ili kuepusha hasira na chuki za kisiasa dhidi yake kutoka kwa waumini na wafuasi wa madhehebu ya kiislamu nchini.”

Habari kwamba muswaada huu umeondolewa bungeni, zimepatikana, huku viongozi wa madhehebu ya Kiislamu –  Masheikh, Waalimu na Wanawazuoni – wakiwa wameupinga kambi mjini Dodoma, kusbiri wanachoita, “ujio wa Mahakama ya Kadhi.”

Hata hivyo, katika hali ambayo imeacha wengi midomo wazi, hadi Ijumaa mchana, serikali ilikuwa bado haijaeleza waumini hao wa Kiislamu kuwa imeuondoa muswaada huo bungeni.

Kwa mujibu wa nadishi la CCM, chama hicho kinasema,

“Katika hali hiyo, CCM kinaweza kucheza siasa za chini kwa chini, tena kwa siri kubwa, za kuwatumia maaskofu kutoka jumuiya na taasisi mbalimbali za kidini nje ya uislamu, kuupinga muswada huo.”

Andishi linasema, “Hii ni kwa sababu, muswaada huu, ukipitishwa na viongozi wa dini za kikristo wakachukia, ‘sumu’ yao kisiasa ni mbaya zaidi kuliko ya viongozi wa kiislamu.”

error: Content is protected !!