January 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Rais Kikwete ampamba Spika Makinda

Spika Anne Makinda

Spread the love

RAIS Jakaya Kikwete amemwagia sifa kedekede Spika wa Bunge Anne Makinda akisema kuwa amelitumikia vizuri bunge na kuliongoza kwa weledi kipindi chote alichoshika nafasi hiyo.

Kikwete amesema hayo leo jioni wakati wa kuhutubia Bunge la mwisho la 10 la serikali yake kwa kipindi chote cha serikali ya awamu ya nne. Anaandika Sarafina Lidwino … (endelea).

Kikwete ambaye leo amesema anatarajia kulivunja bunge hilo rasmi agosti 20 mwaka huu amemwagia Makinda sifa wakati watetezi wa utawala bora nchini wakilalamikia kitendo cha Spika huyo kuwatimua wabunge wa UKAWA kutoka katika bunge hilo la kumi bila kufuata kanuni za Bunge.

Wabunge hao wa UKAWA walitimuliwa baada ya kuhoji uhalali wa maamuzi ya Spika Makinda kutaka Bunge lijadili na kupitisha kwa mpigo miswada mitatu ya sheria za mafuta na gesi asilia.

Kwa maoni ya wabunge wa UKAWA uamuzi huo ni kinyume cha Kanuni za Bunge zilizopo sasa hivi.

Kwa upande mwingine, Rais Kikwete amesema, licha ya kuwepo kwa matukio mengi ya vitisho vya uvunjifu wa amani, chuki, migogoro ya kidini na kuwepo kwa migogoro kati ya Tanzania na Zanzibar lakini viongozi wa Serikali walijitahidi kudhibiti hilo.

Kikwete ameendelea kujinadi kuwa, katika kipindi chake ameboresha na kuongeza vitu vingi vya kimaendeleo yakiwemo ya , kujenga nyumba za Wanajeshi, kupanua magereza, kupambana na waharifu,kuongeza mishahara kwa watumishi wa kiserikali.

“Tumekomesha mianya ya kupenya kwa rushwa, tumeimarisha tume ya haki za binadamu na utawala bora, kuongeza vyuo vya ufundi, kupunguza matumizi mabaya ya serikali na mengine mengi.” Amesema Kikwete

Ameendelea kusema mafanikio makubwa waliyopata ni pamoja na pato la matumizi kuongezeka, upanuzi wa migodi, kupeleka umeme vijijini, kuongezeka kwa wilaya, pamoja na kuwapandisha vyeo watumishi wa serikali.

Amewapoangeza amewapongeza wabunge kwa ushirikiano na kujituma kwao katika kipindi chote, “mimi naamini bila nyinyi serikali haijakamilika. Naondoka au tunaondoka lakini nchi yetu ikiwa ipo salama naondoka nikiwa najiamini” .

Japo bado kunabaadhi ya vitu ambavyo kwa kiasi kidogo tumefeli ikiwemo ya ajali barabarani, maji na vingine ambavyo bado tulikuwa tunandelea nanyo lakini tumejitaidi” amesema Kikwete.

Hata hivyo, katika Bunge hilo wamehudhuria viongozi mbalimbali wan chi akiwemo, Makamo wa Rais Dk.Gharib Bilal, Rais mstaafu Benjamin Mkapa, Ally Hassan Mwinyi, Joseph Waioba, Rais wa Zanzibar Dk. Ally Mohamed Shein Mke wa Rais Mama Salma Kikwete na wengine wengi.

error: Content is protected !!