December 8, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Rais Kikwete akana kujiongezea muda

Rais Jakaya Kikwete akihutubia wananchi

Spread the love

RAIS Jakaya Kikwete, amesema hakuna mpango wa kujiongeze muda madarakani kama inavyodaiwa na vyama vinavyounda kundi la Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa). Anaandika Mwandishi wetu … (endelea)

Kauli ya Kikwete inakuja siku moja baada ya wenyeviti wa vyama hivyo, Freeman Mbowe (Chadema), Prof. Ibrahim Lipumba (CUF), James Mbatia (NCCR-Mageuzi) na Dk. Emmanuel Makaidi (NLD), kudai kuwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), inafanya njama za kumwongeza muda Rais Kikwete.

Ukawa walisema jaribio lolote la kuahirisha uchaguzi mkuu kwa kisingizio chochote kile litakuwa kinyume na Katiba ya sasa na litahesabika sawa na mapinduzi dhidi ya katiba.

Kufuatia madai hayo, Rais Kikwete, katika kuhitimisha hotuba yake kwa wafanyakazi leo jijini Mwanza, aligusia suala hilo akisema ni uongo mtupu kwani hakuna kitu kama hicho.

Baada ya kuwahamasisha wafanyakazi kujitokeza kwa wingi kujiandikisha katika daftari jipya la wapiga kura na kushiriki uchaguzi mku wa Oktoba mwaka huu, Kikwete alisema, “Nimesikia wazee fulani wakisema kuna njama za kuniongeza muda na hivyo uchaguzi hautafanyika.”

Rais Kikwete bila kuwataja walengwa kwa majina, alisita kidogo na kisha kwa tabasamu akasema, “ni uongo mtupu…hakuna kitu kama hicho, na hii ni aibu kwao kusema mambo ambayo hayapo ya kuwatia hofu wananchi.”

Katika madai yao jana, Ukawa kupitia kwa Prof. Lipumba, walisema “NEC haijaanza maandalizi yoyote kwa ajili ya uchaguzi mkuu licha ya kwamba imebaki miezi sita tu kwa mujibu wa Katiba.”

Alisema shughuli zinazohusiana na maandalizi ya uchaguzi mkuu na vifaa vinavyotumika ambavyo kwa taratibu za miaka yote huanza kufanyika angalau mwaka mmoja na nusu kabla ya uchaguzi, hazijaanza kufanyika, vifaa vinavyoohitaji havijanunuliwa na fedha kwa ajili hiyo hazijategwa hadi sasa.

“Serikali ya CCM haijatoa fedha kwa NEC kwa ajili ya uchaguzi mkuu. Badala yake NEC imeendelea kutangaza kwamba inafanya maandalizi kwa ajili ya kura ya maoni kuhusu Katiba Inayopendekezwa ambayo imepitwa muda kisheria,” anasema.

error: Content is protected !!