January 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Rais Kikwete ajivunia kuinua kilimo

Rais Jakaya Kikwete (kulia) akitazama ukulima wa kisasa wa manasi yanayolimwa kwa ajili ya kuuzwa nje ya nchi katika shmaba la Bomarts Farms Ltd.

Spread the love

RAIS Jakaya Kikwete amejitapa kuwa ametimiza ndoto yake ya kuinua sekta ya kilimo ikiwa ni pamoja na kuanzisha benki ya maendeleo ya kilimo Tanzania (TADB), ili kuwainua wakulima wadogo na kuondoa umaskini nchini.  Anaandika Sarafina Lidwino … (endelea).

Amedai, mbali na kuanzisha benki hiyo ameboresha miundo mbinu ikiwemo barabara na kupeleka umeme vijijini ambamo ndicho kilikuwa kilio cha wakulima wengi.

Amesema kuwa katika muda wake aliokaa madarakani amekuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha sekta ya kilimo inapewa kipau mbele ili pindi anapomaliza muda wake taifa lisife njaa.

“Nimejitaidi kupigania sekta hii ili ninapong’atuka nihakikishe umaskini unapungua kwa kuwa sekta ya kilimo ni moja ya sekta muhimu ambayo inaingizia serikali kipata zaidi ya asilimia 25 nataka liongezeke na sikupungua”. Amesema Rais Kikwete.

Hayo ameyasema leo Jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa TADB uliofanyika katika Ukumbi wa Mwalimu Nyerere ambapo amewaambia wanachi dhumuni kubwa la kuanzisha benki hiyo ni kuwafanya watu waitambue sekta hiyo kama ni ajira kama zingine.

Kikwete amesema, licha na jitihada zake za kuwainua wakulima lakini katika upande wa uzalishaji bado wakulima wapo nyuma kulinganisha na nchi nyingine zilizoendelea.

Amesema, mwaka 2006 alipoingia madarakani amewahi kufanya uchambuzi wa changamoto zinazowakabili wakulima   na sekta ya kilimo kwa ujumla na kubaini vitu vinne ambavyo amedai vikitatuliwa sekta yakilimo itainuka.

Amedai vitu hivyo kuwa ni, uhaba wa pembe jero yakiwemo majembe ya kulimia kwa kutumia ng’ombe, umwagiliaji bila ya kutegemea mvua, utumiaji wa mbegu asiliapasipokutumia nguvu nyingi, na utumiaji wa mbolewa za kukuzia mazao.

“Wakulima tukizingatia vitu hivi na kupata ufumbuzi wa haya basi tija ya kilimo itaongezeka na umaskini utapungua.Pia watu watakiheshimu kilimo kama kazi nyingine na kuondoa ile dhana ya kilimo ni kwaajili ya watu wasiosoma au kukosa ajira”. Amesema Kikwete.

Kwa upande wake Waziri wa Fedha Saada Mkuya amesema serikali iliona umuhimu wa kuanzishwa kwa benki hiyo ili kupunguza umaskini nchini.

Amewataka wakulima ambao ndio wahusika wakuu wa benki hiyo, hivyo waitumie vizuri fursa hiyo ili kujikwamua na umaskini.

Akielezea hali ya benki hiyo, Mkurugenzi mwendeshaji wa TADB, Thomas Samkyi amesema, benki hiyo ilianzishwa mwaka 2008 na kukamilika mwaka 2014, ikiwa na wafanyakazi 18 ambapo mpango kazi wake unatarajiwa kuwa hadi mwaka 2020.

Samkyi amesema, benki ka sasa ipotayari kuanza kazi baada ya maandalizi ya mwaka mzima na tayari imepatiwa leseni na benki kuu ya Dunia.Ambapo serikali imetoa pesa kiasi cha Billion 60 za kuanzia.

“Kwa sasa benki inawafanya kazi 45 lakini bado tunaitaji wengi zaidi, pia serikali imeahidi kutoa Billion 800 kwaajili ya kuongeza mtaji na mikopo kwa wakulima”.

Amesema, mtaji huo uliopo, utatumika kuwakopesha wakulima, kubolesha sekta ya kilimo, kuwapatia vijana ajira na kuwainua wanawake wakulima ambapo watapata fursa ya kurejesha fedha hizo baada ya mavuno.

Aidha, benki hiyo kwa sasa ipo maeneo ya kinondoni Dar es Salaam, ambapo inatarajiwa kufika katika kanda zotemikoani na kuanzisha matawi mengine vijijini. Kwa sasa wakulima watapatiwa mikopo hiyo kupitia vikundi vya kuweka na kukopa Saccos.

error: Content is protected !!