
Rais Kikwete akiwa na wachezaji wa Taifa Stars
RAIS Jakaya Kikwete amejiondoa kwenye kipigo cha Timu ya Taifa Tanzania ‘Taifa Stars’ baada ya kusema kuwa yeye siyo sehemu ya timu hiyo kushindwa kufanya vizuri katika mechi za timu hiyo.
Kikwete amesema kuwa alikuwa ni mmoja wa mashabiki wa timu hiyo lakini kutokana na kufanya vibaya kwa timu hiyo, “… niliambiwa kuwa timu inafanya vibaya kutokana na mimi kwenda uwanjani, nikaamua kuacha, lakini cha ajabu bado tunafungwa.
“Pamoja na kuacha kwenda uwanjani, lakini bado tunafungwa, tena hata wakienda nje ya Dar es Salaam bado tunafanya vibaya. Wameenda Zanzibar wamepigwa tatu.”
Kikwete amesema pamoja na kufanya vibaya kwa timu hiyo lakini bado anaisapoti timu hiyo kwa kuwa na ushirikiano ya kituo cha michezo cha Symbion, pamoja na kuanzisha vituo mbalimbali vya soka ili kujenga misingi ya soka la vijana.
Rais Kikwete amesema kutokana na kuboronga kwa timu ya taifa, amewezeka pia kwenye tasnia ya filamu ‘Bongo Movie’ na wasanii wa kizazi kipya ‘Bongo Fleva’ ambao kwa sasa wakiwaliwaza.
“Nimewapa studio wasanii wa Bongo Fleva ambayo imewasahisishia kazi zao, lakini pia kwa upande wa Bongo Movie nimewaleta waandaaji na waigizaji kutoka Marekani ili wabadilishane mawazo. Sitaishia hapo nitaongeza juhudi ili niwaache wakiwa pazuri,” amesema Rais Kikwete.
More Stories
Tiger Wood apata ajali mbaya, alazwa ICU
Simba yaweka rekodi dhidi ya kocha wa Al Ahly
Simba yaifanyia mbaya Al Ahly