December 1, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Rais Kenyatta, Ruto wagongana jukwaa moja Mashujaa Day

Spread the love

 

IKIWA imepita miezi mitatu na ushee kwa Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta na Naibu wake, William Rutto kutoonana ana kwa ana, jana ilikuwa siku ya kipekee kwa viongozi hao wawili kukutana na kukaa jukwaa moja katika siku ya Mashujaa. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Wawili hao sambamba na kinara wa chama kikuu cha upinzani nchini – ODM, Raila Odinga, walikutana katika Kaunti ya Kirinyaga wakati wa maadhimisho hayo ya 58 ya siku ya Mashujaa yaliyofanyika katika uwanja wa Wang’uru jana tarehe 20 Oktoba, 2021.

Kenyatta na Ruto hawajaonana ana kwa ana tangu tarehe 1 Juni, mwaka huu wakati wa maadhimisho ya siku ya Madaraka yaliyofanyika kaunti ya Kisumu nchini humo.

Hivi majuzi Ruto alisema kwamba alismaidia Uhuru na Raila kupata uongozi ila ameshangaa kuona wameungana pamoja kumpinga.

Trehe 23 Agosti, 2021, Uhuru alimueleza Ruto hadharani kwamba ajiuzulu wadhifa wake iwapo hajaridhishwa na namna kazi imekuwa ikitekelezwa badala ya kumkosoa akiwa ndani ya serikali.

Viongozi wengine ambao walihudhuria katika hafla hiyo ya jana ni pamoja na viongozi wa vyama mbalimbali vya siasa nchini humo ikiwamo ANC, Musalia Mudavadi, Kiongozi wa KANU, Gideon Moi, Kiongozi wa Narc-Kenya, Martha Karua na Jaji Mkuu wa nchi hiyo, Martha Koome.

error: Content is protected !!