Thursday , 30 March 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Rais Kenyatta atuma ujumbe Tanzania, Samia atoa maagizo
Habari za SiasaTangulizi

Rais Kenyatta atuma ujumbe Tanzania, Samia atoa maagizo

Spread the love

 

RAIS wa Tanzania, amewataka mawaziri na wataalamu wa Tanzania na Kenya wanaounda Kamati ya Ushirikiano wa Pamoja, kukutana mara moja ili kufanyia kazi masuala mbalimbali ya uhusiano. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Kamati hiyo, ilikutana mara ya mwisho mwaka 2016.

Ametoa maagizo hayo leo Jumamosi tarehe 10 Aprili 2021, Ikulu jijini Dar es Salaam, baada ya kupokea ujumbe maalum kutoka kwa Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya uliowasilishwa na Waziri wa Michezo, Utamaduni na Urithi wa Kenya, Balozi Amina Mohamed.

Mara baada ya kupokea ujumbe huo, Rais Samia, amefanya mazungumzo na Balozi Amina, kuhusiana na dhamira ya Tanzania na Kenya kuendeleza na kukuza zaidi uhusiano na ushirikiano katika nyanja mbalimbali hususani kiuchumi na kijamii.

Taarifa iliyotolewa na Gerson Msigwa, Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, imesema Balozi Amina ameongozana na Balozi wa Kenya nchini Tanzania, Dan Kazungu.

Pia, mazungumzo hayo, yamehudhuliwa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania, Balozi Liberata Mulamula na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Hussein Kattanga.

Rais Samia amemhakikishia, Rais Kenyatta kuwa Serikali anayoiongoza ipo tayari kuendeleza mambo mazuri yote yaliyokuwa yakifanywa na mtangulizi wake Hayati John Pombe Magufuli na kutatua changamoto kati ya Tanzania na Kenya.

Amesema, nchi hizo za Jumuiya ya Afrika Mashariki ni ndugu, majirani na marafiki wa kihistoria.

Rais Kenyatta amemwalika Rais Samia kufanya ziara rasmi nchini Kenya ili kukuza zaidi uhusiano na ushirikiano.

Amemhakikishia Rais Samia kuwa Kenya ipo tayari wakati wote kushirikiana na Tanzania kwa kuendeleza na kukuza zaidi ushirikiano kati ya nchi hizo.

Hayati Magufuli, alifariki dunia tarehe 17 Machi 2021, katika Hospitali ya Mzena, Dar es Salaam na mwili wake, kuzikwa nyumbani kwao Chato mkoani Geita.

Baada ya kifo hicho, Samia aliyekuwa makamu wa Rais, aliapishwa kuwa Rais wa Tanzania, tarehe 19 Machi 2021.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

TEMESA iliyokarabati Kivuko kwa Bil 7.5 yapata hati chafu

Spread the love  MDHIBITI na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG),...

Habari za Siasa

ACT-Wazalendo yakusanya Mil 8.5/- kodi ya zuio na kutokomea nazo

Spread the love  MDHIBITI na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG),...

Habari za Siasa

DC Kasilda Mgeni ahamasisha chakula shuleni

Spread the love  MKUU wa Wilaya ya Same, mkoani Kilimanjaro, Kasilda Mgeni...

Habari za Siasa

Bilioni 223.9 zapelekwa Tunduru ndani ya miaka 2 ya SSH

Spread the love  ZAIDI ya Sh. bilioni 223.9 zimepelekwa Wilaya ya Tunduru...

error: Content is protected !!