UHURU Kenyatta, Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta, ametoa siku 14 kwa mawaziri wake, kuhakikisha mahindi kutoka Tanzania, yaliyokwama mpaka wa Namanga, mkoani Arusha yanaondoka. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).
Rais Kenyatta, ametoa agizo hilo, leo Jumatano, tarehe 5 Mei 2021, mbele ya Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, wakati akizungumza katika Jukwaa la Wafanyabiashara, kati ya Tanzania-Kenya.
Ni katika siku ya pili na ya mwisho ya ziara ya Rais Samia nchini Kenya, aliyoianza jana Jumanne na ataihitimisha leo Jumatano na kurejea nchini mwake Tanzania.
Agizo hilo, amelitoa ikiwa ni takribani miezi miwili, malori yenye shehena ya mahindi, yamekwama kwenye mpaka wa Namanga.
Ni baada ya Kenya, kupiga marufuku ununuzi wa mahindi kutoka mataifa jirani ya Tanzania na Uganda kutokana na kile kinachoelezwa kwamba mahindi kutoka nchi hizo mbili sio salama kwa matumizi ya binadamu.
Taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi mkuu wa mamlaka ya kilimo na chakula wa nchini Kenya wakati zuio hilo linatolewa, ilieleza mahindi hayo yana kiwango kikubwa cha sumu kuvu, ambayo ni hatari kwa usalama wa walaji.
Leave a comment