July 29, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Rais Kagame mgeni rasmi Sabasaba

Spread the love

PAUL Kagame, Rais wa Rwanda anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa maonesho ya 40 ya biashara ya kimataifa (Sabasaba) yanaotarajiwa kuanza kufanyika Julai Mosi mwaka huu, anaandika Regina Mkonde.

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kukabidhiwa msaada wa madawati kutoka kwa Jassem Al-Najem, Balozi wa Kuwait nchini Tanzania, Balozi Augustino Mahiga, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki amesema, Rais John Magufuli amemtumia barua ya mualiko.

“Kwa mara ya kwanza Rais Kagame atasaini mkataba wa makubaliano ya uwekezaji kwenye sekta mbalimbali zilizopo katika nchi hizo mbili.Pia anatarajiwa kuwa mgeni rasmi na mzinduaji wa maonesho ya biashara ya kimataifa ya sabasaba,” amesema Mahiga.

Amesema ujio wa Kagame unalenga kuimarisha mahusiano mazuri baina ya nchi ya Rwanda na Tanzania hususan katika mahusiano ya kiuchumi.

Aidha, Mahiga amesema kuwa madawati aliyoyapokea yatasaidia kuondoa changamoto ya uhaba wa madawati na kwamba wanafunzi watapata muamko wa kufuatilia masomo yao.

“Changamoto ya uhaba wa madawati ilongezeka baada ya tamko la rais la kutoa elimu bure kuanzia shule ya msingi hadi sekondari, na kwamba msaada huu utasaidia kupunguza changamoto hiyo na kuboresha elimu” amesema.

Mhaiga amesema uboreshwaji wa elimu utasaidia kuchochea mafanikio ya sekta ya viwanda kwa kuwa elimu ndiyo nyenzo muhimu katika sekta hiyo.

“Katika kuelekea uchumi wa viwand nyenzo pekee ya kufanikisha mpango huo ni elimu kwa kuwa hakuna uwekezaji mzuri wa rasilimali wenye tija kama kuwkeza elimu kwa vijana,”amesema.

error: Content is protected !!