RAIS wa Rwanda, Paul Kagame, amedai kwamba Serikali yake haichochei mgogoro wa kivita unaoendelea mashariki mwa nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa…(endelea).
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na BBC Swahili, Rais Kagame ametoa kauli hiyo jana Jumatano, akiwa nchini Marekani, alipoulizwa na waandishi wa habari kuhudu hatua ambazo Serikali yake inazichukua, kukomesha mauaji ya raia yanayoendelea kutokea katika vita hiyo.
Swali hilo limekuja baada ya Rais wa DRC, Felix Tshisekedi, katika mkutano wa wakuu wa nchi za Afrika na Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Antony Blinken, uliofanyika Jumanne, kudai vita inayoendelea nchini mwake inachochea kwa siri na Rwanda.
“Tatizo halikuanzishwa na Rwanda na sio tatizo la Rwanda, ni tatizo la Congo,” Rais Kagame alikanusha madai hayo.
Kwa muda mrefu Serikali ya Rwanda imekabiliwa na tuhuma za kuwaunga mkono ikiwemo kuwapa silaha waasi wanaopigana na vikosi vya ulinzi na usalama vya DRC.
Leave a comment