January 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Rais Jakaya Kikwete aenda Rwanda

Rais Paul Kagame (kulia) na Rais Jakaya Kikwete

Spread the love

RAIS Jakaya Kikwete ameondoka nchini asubuhi ya leo, kwenda Kigali, Rwanda kwa ziara ya siku moja nchini humo kwa mwaliko wa Rais Paul Kagame.

Taarifa ya Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais-Ikulu, imesema kuwa, wakati akiwa Kigali, miongoni mwa mambo mengine, Rais Kikwete atahudhuria mkutano wa tisa wa wakuu wa nchi kujadili miradi iliyoko katika Ukanda wa Kaskazini unaofanyika leo katika Hoteli ya Serena mjini Kigali.

Mkutano wa huo unatarajiwa kuhudhuriwa na marais Uhuru Kenyatta (Kenya), Yoweli Museven (Uganda) na wenyeji Kagame huku marais Salva Kiir (Sudan Kusini) na Pierre Nkuruzinza wa Burundi nao wakihudhuria kama waalikwa.

Lengo la mkutano huo ni kujadili hatua za utekelezaji wa miradi mbali mbali iliyokubaliwa kulingana na maelekezo yaliyotolewa katika mkutano wa nane wa namna hiyo uliofanyika Nairobi, Kenya, Desemba 11, mwaka jana, 2014.

Rais Kikwete atarejea nchini jioni ya leo baada ya kumalizika kwa mkutano huo.

error: Content is protected !!