MAHAMADOU Issoufou, Rais Mstaafu wa Niger, ametunukiwa tuzo ya Mo Ibrahimu inayoonesha Ufanisi katika Uongozi kwa Afrika. Inaripoti mitandao ya kimataifa…(endelea).
Rais Issoufou aliteuliwa kutwaa tuzo hiyo baada ya kikao cha Kamati Huru ya Tuzo hiyo kukutana jana Jumatatu tarehe 8 Machi 2021.
Taarifa kutoka kwenye kamati hiyo imeeleza, miongoni mwa kilichoisukuma kumteua kiongozi huyo ni pamoja na kulisaidia taifa lake kiuchumi wakati wa utawala wake (2011-2020).
Rais Issoufou amekuwa kiongozi wa sita kupokea tuzo hiyo ya heshima Afrika kwa viongozi wastaafu wa mataifa yao.
Kiongozi huyo pia, amesifiwa na kamati hiyo kwa kuimarisha demokrasia sambamba na kulinda utawala wa sheria. Na kwamba, wakati akichukua, nchi hiyo ilikuwa katika uchumi duni.
Festus Mogae, mwenyekiti wa hamati hiyo ambaye ni Rais Mstaafu wa Botswana amesema, Rais Issoufou alisimama imara wakati nchi yake ikipita kwenye misimamo mikali ya vurugu, kuongezeka kwa jangwa pamoja na hali mbaya ya kisiasa.
Leave a comment