Saturday , 20 April 2024
Home Gazeti Habari Rais Dk. Mwinyi: Watanzania tusibaki watazamaji katika uwekezaji
Habari

Rais Dk. Mwinyi: Watanzania tusibaki watazamaji katika uwekezaji

Dk. HUssein Mwinyi, Rais wa Zanzibar
Spread the love

 

RAIS wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Dk. Hussein Ali Mwinyi ametoa wito kwa Watanzania kushirikia kikamilifu katika harakati za uwekezaji nchini badala ya kubaki kuwa watazamaji. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea)

Amesisitiza kuwa viongozi wa Serikali za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Zanzibar wanapozungumzia uwekezaji isieleweki kuwa wanazungumzia watu kutoka nje tu.

“Tungependa Watanzania na Wazanzibar wakashiriki wasiwe watazamaji, kwa hiyo serikali itachukua kila hatua kuhakikisha wananchi wetu wa ndani wanashiriki kikamilifu na hatubaki kuwa watazamaji,” amesema.

Dk. Mwinyi ametoa kauli hiyo leo tarehe 7 Disemba 2021, Visiwani Zanzibar katika ufunguzi wa kongamano la maonesho ya bidhaa za viwanda.

Kongamano hilo ni maalumu katika kujadili changamoto na mafanikio ya maendeleo ya uwekezaji kwa kipindi cha miaka 60 tangu Tanzania ipate uhuru mwaka 1961.

Pamoja na mambo mengine amewashauri wafanyabiashara wa Tanzania kwamba kupitia jumuiya zao wawe karibu na serikali ili waweze kufanya kazi kwa pamoja.

Amesema Serikali ya awamu ya nane tangu ilipoingia madarakani imechukua jitihada za kuimarisha Mamlaka ya Kukuza Uwekezaji Zanzibar (ZIPA) ili kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa majuku yake.

Amesema utendaji wa ZIPA umeimarishwa baada ya kuanzishwa kituo cha pamoja kinachotoa huduma za uwekezaji, zikiwemo zinazohusu vibali vya ukaazi, vibali vya ujenzi, usajili wa makampuni, masuala ya kodi na mazingira.

Amesema hivi sasa ikiwa mwekezaji atakamilisha vema taratibu kabla ya kwenda kituoni ataweza kupata kibali ndani ya siku tatu lakini lengo la Serikali kuhakikisha kibali cha uwekezaji kipatikana ndani ya saa 24.

Aidha, katika suala la kutatua tatizo la upatikanaji wa ardhi kwa ajili ya uwekezaji, Serikali ya Zanzibar inakamilisha zoezi la uwepo wa benki ya ardhi, pamoja na mambo mengine tutabainisha maeneo ardhi yaliyotengwa kwa ajili ya uwekezaji.

“Katika jitihada za kuimarisha uwekezaji Zanzibar, serikali imetangaza fursa za uwekezaji katika visiwa vidogo 10 vilivyopo hapa Zanzibar, zoezei la kuwapata wawekezaji linaendelea.

“Serikali inaendelea kuhamasiasha uwekezaji kati ya serikali na sekta binafsi katika sekta mbalimbali zikiwemo za afya, kilimo, ufugaji, uvuvi, nishati na miundombinu.

“Fursa za uwekezaji zipo pia katika uvuvi wa bahari kuu, viwanda na ujenzi wa nyumba za makazi na biashara,” amesema.

Amesema katika kufanikisha utekelezaji wa uchumi wa bluu ambao ndio ajenda maalumu, serikali inakaribisha wawekezaji mbalimbali katika utekelezaji wa miradi inayohusiana na uchumi huo wa bahari.

Ameitaja miradi hiyo kuwa ni ujenzi wa bandari kubwa ya kisasa ya Mangapwani, ambayo itajumuisha ujenzi wa bandari ya makontena, mafuta na gesi, nafaka na chelezo kwa ajili ya matengenezo ya meli.

Amesema eneo hilo pia litakuwa na mji wa kisasa na huduma mbalimbali.

Aidha, katika kuendeleza uchumi wa bahari tunawakaribisha wawekezaji kuja kuwekeza kwenye sekta ya utalii ambayo ina fursa nyingi hapa Zanzibar.

Amesema jitihada kama hizo za kuimarisha mazingira ya uwekezaji pia zinafanywa upande wa Bara.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

HabariSiasa

Dk. Rose Rwakatare atoa kadi 500 kila Wilaya Morogoro

Spread the loveMWENYEKITI wa Jumuiya ya Wazazi CCM Mkoa wa Morogoro, Dk...

ElimuHabari

CBE, WMA wasaini makubaliano wanafunzi kusoma wakifanyakazi

Spread the loveNAIBU Spika Musa Azzan Zungu amekipongeza Chuo cha Elimu ya...

HabariTangulizi

Dk. Slaa, Mwabukusi kuhojiwa na jeshi la Polisi Mbeya

Spread the loveJESHI la Polisi jijini Mbeya, linawashikilia kwa mahojiano Dk. Wilbroad...

HabariHabari Mchanganyiko

Kairuki Hospital Green IVF  yawanoa madaktari kuhusu upandikizaji mimba

Spread the love KITUO cha Upandikizaji Mimba cha Kairuki Hospital Green IVF...

error: Content is protected !!