Friday , 19 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Rais Dk.Mwinyi aongoza mamia ya wananchi maziko ya kaka yake
Habari Mchanganyiko

Rais Dk.Mwinyi aongoza mamia ya wananchi maziko ya kaka yake

Spread the love

 

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi leo tarehe 31 Agosti, 2022 amejumuika na viongozi wa kitaifa, vyama vya kisiasa pamoja na mamia ya wananchi katika maziko ya kaka yake, Hassan Ali Mwinyi yaliofanyika Mangapwani Mkoa Kaskazini Unguja. Anaripoti Mwandishi Wetu, Zanzibar … (endelea).

0Marehemu Hassan Ali Mwinyi (66) alifariki dunia jana usiku katika Hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja jijini Zanzibar alikokuwa amelazwa kwa kipindi kirefu.

Maandalizi ya maziko ya marehemu Hassan yalifanyika nyumbani kwake Chukwani Mkoa Mjini Magharibi, ambapo wananchi, ndugu na jamaa pamoja na majirani walipata fursa ya kumswalia na baadae mwili wake kusafirishwa hadi Mangapwani, ambako aliswaliwa tena na hatimaye kuzikwa kwenye shamba la familia.

Akitoa nasaha baada ya kukamilika kwa hafla ya dua na sala, Mjumbe wa Maulamaa Mkoa Kaskazini Unguja, Sheikh Khamis Abdulhamid aliwataka waislamu kumuombea maghfira marehemu huyo, huku akiitaka familia kuwa na moyo wa subira.

Naye Balozi wa Tanzania nchini Saud Arabia, Ali Mwadini akiwasilisha salamu kwa Rais mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Alhaj Ali Hassan Mwinyi, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk.Mwinyi pamoja na wanafamilia, kwa niaba ya mabalozi hao, alimuombea maghfira kwa Mwenyezi Mungu marehemu huyo.

p
Aidha, akitoa salamu kwa niaba ya Kikosi Kazi Tanzania, Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Sheikh Alhad Mussa alitoa pole kwa familia ya marehemu pamoja na kumuombea marehemu maghfira kwa Mwenyezi Mungu.

Aidha, akitoa shukrani kwa niaba ya familia ya marehemu, ndugu wa marehemu huyo Abdalla Ali Mwinyi aliwashukuru wananchi wote walioungana na familia katika msiba huo mzito wa ndugu yao.

Marehemu Hassan Ali Mwinyi (66) akiwa mtoto wa Pili wa Familia ya Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Alhaj Ali Hassan Mwinyi kutoka uzawa wa Mama Mtumwa Yussuf, ameacha mjane na watoto saba.

Katika kipindi cha uhai wake aliwahi kuwa Mtumishi wa Umma na miongoni mwa nyadhifa alizoshika ni pamoja na Meneja wa Shirika la Meli Zanzibar.

Viongozi mbalimbali wa Kitaifa walishiriki maziko hayo akiwemo Rais mstaafu wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Abeid Amani Karume, Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Othman Masoud Othman, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Hemed Suleiman Abdulla, Waziri Mkuu mstaafu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mizengo Pinda pamoja na viongozi mbalimbali wa Serikali ya SMZ,SMT na masheikh.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB Pesa Akaunti yawavutia wakaguzi wa ndani Afrika

Spread the loveUbunifu wa bidhaa bora wa Benki ya NMB pamoja na...

Habari Mchanganyiko

Carbon First, Ruangwa wasaini makubaliano ya biashara ya hewa ukaa

Spread the love  KAMPUNI ya Carbon First Tanzania Limited na Halmashauri ya...

Habari Mchanganyiko

CBE yawakumbuka wenye mahitaji maalum Jangwani

Spread the loveCHUO cha Elimu ya Biashara (CBE), kimetoa msaada mbalimbali na...

Habari Mchanganyiko

Mume auwa mke kwa kumchoma visu, ajisalimisha Polisi

Spread the loveJACKSON Kalamji (49), anashikiliwa na Jeshi la Polisi jijini Mwanza,...

error: Content is protected !!