September 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Rais Burkina Faso awekwa kizuizini

Spread the love

Rais wa Burkina Faso, Roch Marc Christian Kaboré amezuiliwa katika kambi ya jeshi nchini humo. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Kwa mujibu wa Shirika la habari la Reuters ni kwamba milio ya risasi ilisikika jana jioni tarehe 23 Januari, 2022 karibu na makazi ya rais wa Burkina Faso.

Inaelezwa kuwa hayo yamejiri baada ya wanajeshi kuasi katika kambi kadhaa wakidai kuondolewa kwa viongozi wakuu wa kijeshi na kuwezeshwa zaidi katika mapambano dhidi ya waasi wa Kiislamu.

Hata hivyo, serikali imekanusha uvumi juu ya mapinduzi hayo

Waandamanaji wanaopinga namna serikali inavyoshughulikia uasi wa wafuasi wa itikadi kali, waliyachoma moto makao makuu ya chama tawala mjini Ougadougou.

Siku ya Jumamosi, wanajeshi wasiopungua wawili waliuawa na wengine kadhaa kujeruhiwa katika mlipuko wa bomu lililotengenezwa kienyeji, kwenye barabara kati ya Ouahigouya na Titao (Kaskazini).

Mlipuko huo ulitokea wakati gari lao lililokuwa likiwasindikiza wafanyabiashara lilipokanya bomu hilo.

error: Content is protected !!