Monday , 30 January 2023
Home Kitengo Habari Kimataifa Rais Biden amteua mwanamke ‘muafrika’ kuwa jaji wa mahakama ya juu
Kimataifa

Rais Biden amteua mwanamke ‘muafrika’ kuwa jaji wa mahakama ya juu

Spread the love

RAIS wa Marekani, Joe Biden amemteua mwanamke wa kwanza mweusi kuwa jaji wa Mahakama ya Juu kabisa nchini humo. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa … (endelea).

Ketanji Jackson ambaye ni jaji katika Mahakama ya Rufaa anakuwa mwanamke wa kwanza mweusi kwenye mahakama hiyo ambayo awali ilitangaza kwamba hastahili kupata uraia wa nchi hiyo kutokana na rangi ya ngozi yake na hivyo kuidhinisha ubaguzi.

Biden anatekeleza ahadi yake ya kampeni ya kuweka historia ya mtu atakayemtangaza kushika nafasi hiyo, na kuongeza sura tofauti kwenye mahakama ambayo imetawaliwa na wanaume wazungu kwa takriban miongo miwili.

Iwapo ataidhinishwa atakuwa mwanamke wa sita kuhudumu kwenye mahakama hiyo pia atakuwa mwanamke wa kwanza mweusi kuhudumu kwenye nafasi hiyo katika historia ya miaka 233 ya mahakama hiyo.

Hatua hiyo itamaanisha kwamba kwa mara ya kwanza majaji wanne wanawake watakuwa miongoni mwa jopo la majaji tisa.

Rais Biden alimwagia sifa Jackson kuwa ni mmoja wa wanasheria wenye uwezo wa juu wa masuala ya sheria nchini humo.

Atachukua nafasi ya Jaji wa Mahakama Kuu Stephen Breyer wakati atakapostaafu mwishoni mwa muhula wa mahakama mwezi Juni.

Wakati baraza la seneti likigawanyika kwa wajumbe 50-50 kati ya vyama vya Republican na Democrats, inatajwa Democrats kuwa na kura za kutosha kuthibitisha chaguo hilo la Rais Biden iwapo wote watamuunga mkono.

Aidha, Makamu wa rais Kamala Harris kutoka Democrats ana kura ya turufu iwapo bunge litapiga kura na kufungana.

Mahakama Kuu ina jukumu muhimu katika maisha ya wamarekani na mara nyingi imekuwa na neno la mwisho juu ya sheria zenye utata, migogoro kati ya majimbo na serikali ya shirikisho, na maamuzi ya rufaa za mwisho zitaendelea kwenye utekelezaji.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Kimataifa

DCI ajitosa uchunguzi matokeo uchaguzi mkuu Kenya

Spread the loveOFISI ya Mkurugenzi ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI)...

HabariKimataifa

Aliyesomeshwa na mchumba aamuriwa kurudisha Sh 9.4 Mil. baada ya kukataa kuolewa

Spread the love  MWANAMKE mmoja nchini Uganda ambaye aliuumiza moyo wa mchumba...

Kimataifa

Uganda yaanza kuchimba mafuta

Spread the love  UCHIMBAJI wa kwanza wa mafuta kibiashara nchini Uganda umeanza...

Kimataifa

Afrika kusini waandamana kushinikiza serikali kumaliza tatizo la umeme

Spread the love  MAMIA ya wafuasi wa Chama cha upinzani nchini Afrika...

error: Content is protected !!