December 5, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Rais Benki ya Dunia agoma kujiuzulu

Spread the love

 

RAIS wa Benki ya Dunia, David Malpass amesema kwamba hatajiuzulu kutokana ukosoaji dhidi ya matamshi yake aliyoyatoa kuhusiana na mabadiliko ya tabianchi. Anaripoti Mitandao ya kimataifa … (endelea).

Malpass ametoa kauli hiyo jana tarehe 23 Septemba, 2022 baada ya mapema wiki hii kushindwa kutoa jibu la moja kwa moja alipoulizwa iwapo utoaji wa nishati ya mafuta umechangia ongezeko la joto duniani na badala yake alisema yeye si mwanasayansi.

Katika mahojiano na gazeti la Politico Friday jana Malpass amesema hatajiuzulu na wala hajaombwa kufanya hivyo na serikali yoyote mwanachama wa Benki hiyo.

Aidha, amesema Benki ya Dunia inachukua hatamu ya uongozi katika masuala ya hali ya hewa na kuongeza kuwa ni wazi nishati ya mafuta inayotokana na shughuli za binadamu huchangia mabadiliko ya tabianchi.

error: Content is protected !!