June 30, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Rais atoroka na dola mil 169

Rais wa Afghanistan, Ashraf Ghani

Spread the love

 

RAIS aliyeondolewa madarakani nchini Afghanistan, Ashraf Ghani anadaiwa kubeba dola za Marekani milioni 169. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa … (endelea).

Rais Ghani ambaye sasa imethibitishwa kuwa ametimkia katika Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE), alitoroka Ikulu ya nchi hiyo iliyopo katika mji mkuu wa Kabul baada ya wanajeshi wa kikundi cha Taliban kuuteka mji huo na miji mingine muhimu.

Kwa mujibu wa Mohammad Zahir Aghbar ambaye ni Balozi wa Afghanistan nchini Tajikstan, Rais Ghani alikuwa amebeba fedha hizo alipotoroka nchi yake siku ya jumapili Agosti 15.

Akizungumza na waandishi wa Habari katika mji mkuu wa Tajik Dushanbe, balozi huyo alisema kuondoka kwa Ghani ni sawa na ‘usaliti kwa taifa lake.’

error: Content is protected !!