April 13, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Rais anapotoshwa – LHRC

Rais John Magufuli

Spread the love

ANNA Henga, Mkurugenzi wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), amesema baadhi ya wasaidizi wa Rais John Magufuli, wanampotosha kwa maslahi yao ya kisiasa. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Henga ametoa kauli hiyo tarehe 13 Desemba 2019, wakati alipozungumza na MwanaHALISI ONLINE, kuhusu tuhuma zilizotolewa na Rais Magufuli, kwamba kuna Asasi za Kiraia (AZAKI) na Mashirika Yasiyo ya Kiserikali (NGO’s), zinatumiwa na watu wasioitakia mema nchi.

Akizungumzia tuhuma hizo kwa ufupi, Henga amesema Rais Magufuli anapotoshwa na baadhi ya wasaidizi wake, kuhusu suala hilo.

“Baadhi ya wasaidizi wa Rais wanamuongoza vibaya kwa masilahi yao ya kisiasa,” amesema Henga.

Wakati akifungua semina ya wajumbe wa Halmshauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM), jijini Mwanza, aliekeza tuhuma kwa AZAKI na NGO’S, watu wasioitakia mema Tanzania, watatumia asasi hizo, kujifanya wanafundisha Demokrasia na haki za binadamu.

Wakati wao wanavunja misingi hiyo, kwa kujenga mifumo ya kinyonyaji, kuchochea machafuko na kuingilia uhuru wa mataifa mengine.

error: Content is protected !!