RAIS wa Mali aliyeondolewa madarakani, Ibrahim Boubacar Keita amefariki akiwa na umri wa miaka 76, familia yake na rafiki zake wamesema. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).
Miaka miwili iliopita aliugua kiharusi lakini chanzo cha kifo chake siku ya jana Jumapili tarehe 16 Januari 2022, hajawekwa wazi.
Mmoja wa ndugu zake amelieleza Shirika la Habari la Ufaransa (AFP) kuwa alifariki muda wa saa tatu usiku nyumbani kwake mjini Bamako, nchini Mali.
Keita aliiongoza Mali kwa miaka saba hadi 2020, wakati alipopinduliwa kufuatia maandamano makubwa dhidi ya serikali kutokana na jinsi alivyolishughulikia suala la wapinzani wake.
Mgogoro wa kiuchumi na uchaguzi ulio huru pia ulisababisha maandamano hayo dhidi ya utawala wake.
Keita alihusika katika siasa kwa zaidi ya miongo mitatu, akihudumu kama waziri mkuu kutoka 1994 hadi 2000.
Leave a comment