Wednesday , 27 September 2023
Home Kitengo Habari Kimataifa Rais ajiua kwa risasi kukwepa kukamatwa na Jeshi
Kimataifa

Rais ajiua kwa risasi kukwepa kukamatwa na Jeshi

Spread the love

RAIS Mstaafu wa nchi ya Peru, Alan Garcia amejiua  kwa kujipiga risasi akikwepa kuingia mikononi mwa Jeshi la Polisi la nchi hiyo, kufuatia tuhuma zilizokuwa zina mkabili za kupokea rushwa. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa … (endelea).

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na vyombo vya habari vya kimataifa, inaeleza kwamba Garcia amefariki dunia wakati akipatiwa matibabu kutokana na majeraha ya risasi, katika Hospitali ya Mji Mkuu wa Peru, Lima.

Rais wa Peru, Martin Vizcarra amethibitisha kifo cha mwanasiasa huyo aliye tawala Peru katika kipindi cha mwaka 1985 hadi 1990, na mwaka 2006 hadi 2011.

Waziri wa Mambo ya Ndani wa Peru, Carlos Moran amesema kabla ya Garcia kujipiga risasi, ali waambia maafisa wa polisi waliofika nyumbani kwake kwa ajili ya kumkamata, kwamba anahitaji kupiga simu kwa jamaa yake, aliporuhusiwa alikwenda kujifungia chumbani.

“Dakika chache baadae ulisikika mlio wa risasi, polisi walijaribu kufungua mlango na walipofanikiwa walimkuta Garcia akiwa katika kiti huku akiwa na jeraha la risasi kichwani,” amesema Moran.

Katibu wa marehemu Garcia, Ricardo Pinedo, amesema rais huyo wa zamani alikuwa anamiliki silaha za moto tano nyumbani kwake, na kwamba moja wapo ndiyo alitumia kumaliza uhai wake.

Jeshi la Polisi lilikuwa linamsaka  Garcia likimtuhumu kufanya kosa la kupokea rushwa enzi za utawala wake, kutoka katika kampuni ya Brazil ya Odebrecht inayoshughulika na masuala ya ujenzi.

Taarifa za vyombo vya uchunguzi nchini Peru, zinaeleza kwamba Garcia alipokea rushwa kiasi cha dola za Marekani 30 Milioni kutoka kwa kampuni ya Odebrecht.Hata hivyo, Garcia mara kadhaa alinukuliwa akikanusha tuhuma hizo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Kimataifa

Mahakama yamkuta na hatia Donald Trump

Spread the love  ALIYEKUWA Rais wa Marekani, Donald Trump, amekutwa na hatia...

Kimataifa

Harusi yageuka msiba 100 wakifariki kwa ajali ya moto

Spread the love  WATU takribani 100, akiwemo bibi na bwana harusi, wamefariki...

Kimataifa

Kampuni ya mali ya China Oceanwide yapata agizo la kufilisiwa huko Bermuda

Spread the love  MAHAKAMA ya Bermuda imetoa amri ya kufilisiwa kwa Kamapuni...

Kimataifa

Uvamizi wa kijeshi Milango ya bahari ya Taiwan G7 yapinga China

Spread the loveMKUTANO wa Mawaziri wa Mambo ya nje wa nchi za...

error: Content is protected !!