Friday , 19 April 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Rais aidhinisha sheria inayotoa adhabu miezi sita jela kwa wauguzi wanaogoma
Kimataifa

Rais aidhinisha sheria inayotoa adhabu miezi sita jela kwa wauguzi wanaogoma

Spread the love

 

SERIKALI ya Zimbabwe jana tarehe 10 Januari, 2023 imepitisha muswada wa sheria inayopiga marufuku maandamano yaliyoandaliwa na wafanyakazi wa afya nchini humo kufuatia mgomo katika mzozo wa muda mrefu kuhusu malipo. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa … (endelea).

Kwa mujibu wa Sheria hiyo mpya iliyosainiwa na Rais Zimbabwe, Emmerson Mnangagwa mapema wiki hii, sheria hiyo inapiga marufuku maandamano yaliyoandaliwa na wahudumu wa afya nchini Zimbabwe na kuchukuliwa kuwa ni kosa la jinai hiyvo kuwafanya waandamanaji kukabiliwa na adhabu ya faini au kifungo cha mpaka miezi sita jela.

Sheria hiyo mpya inakuja baada ya vuta nikuvule ya mzozo wa muda mrefu baina na wahudumu wa afya na serikali kuhusu mishahara.

Maelfu ya wauguzi na madaktari katika hospitali zinazosimamiwa na serikali waligoma mwaka jana, na katika miaka ya nyuma, wakidai nyongeza ya mishahara na kutaka kulipwa mishahara hiyo kwa dola za Kimarekani.

Hiyo inatokana na kushuka thamani kwa sarafu ya nchi hiyo na kupanda kwa mfumuko wa bei ulioshusha thamani ya mapato yao kama anavyoeleza Pretty Gudza mmoja wa wauguzi walioandamana.

“Siwezi kulipa kodi yangu, siwezi kula, kwa hivyo hali zetu ni mbaya na sababu ya kufanya mgomo huu ina uhalali,” anasema muuguzi Gudza.

Wauguzi wengi nchini Zimbabwe wanalipwa chini ya dola 100 kwa mwezi.

Taifa hilo la Kusini mwa Afrika limeshuhudia idadi kubwa ya wauguzi na madaktari wanaoondoka hatua ambayo imesababisha hospitali kukosa wafanyakazi.

Novemba mwaka 2022 Bodi ya Huduma za Afya ya Zimbabwe ilisema zaidi ya wafanyakazi 4,000 wa afya wameondoka nchini humo tangu 2021.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

KimataifaTangulizi

Mkuu wa majeshi Kenya afariki, Ruto atangaza maombolezo

Spread the loveRais wa Kenya, William Ruto ametangaza maombezo ya siku tatu...

Kimataifa

Majaji kuamua hatima ya Zuma leo

Spread the loveMajaji nchini Afrika Kusini leo Jumanne wataamua ikiwa rais wa...

Habari za SiasaKimataifa

Spika Afrika Kusini ajiuzulu kwa tuhuma za rushwa

Spread the loveSpika wa Bunge la Afrika Kusini, Nosiviwe Mapisa-Nqakula ametangaza kujiuzulu...

Habari MchanganyikoKimataifa

Tetemeko la ardhi laua 7, lajeruhi 800 Taiwan

Spread the loveWatu wapatao saba wamefariki dunia na wengine zaidi ya 800...

error: Content is protected !!