Sunday , 25 February 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Rais Addo amwibia Clinton, Bush
Kimataifa

Rais Addo amwibia Clinton, Bush

Spread the love

AKIWA na siku tatu ndani ya Ikulu ya Ghana, Rais Nana Akufo Addo anatuhumiwa kuiba sehemu ya hotuba za marais wa Marekani siku ya kuapishwa kwake jijini Accra, anaandika Wolfram Mwalongo.

Mitandao ya kijamii ya nchini humo imemshambulia rais hiyo kwa kunyofoa maneno kwenye hotuba zilizotolewa na aliyekuwa rais wa 42 wa Marekani, Bill Clinton aliyoitoa mwaka 1993 pia Rais wa 43 George Bush aliyoitoa mwaka 2001.

Hata hivyo, Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Rais huyo amekiri kuchotwa kwa baadhi ya maneno kutoka katika hotuba za marais hao wa Marekani.

Ofisi hiyo imeomba radhi kwa umma kutokana na kitendo hicho kilichoanza kuibua mijadala katika mitandao ya kijamii tangu siku ya kuapishwa kwake.

Tukio la aina hii lilitokea mwaka jana katika kampeni za uchaguzi mkuu wa Marekani baada ya Melania Trump, mke wa Donald Trump alipotoa hotuba tarehe 19 Juni mwaka jana iliyofanana na ile iliyotolewa na mke wa Barrack Obama, Michele Obama mwaka 2008. Melania alishambuliwana wafuasi wa Hillary Clinton.

Rais Addo aliapishwa tarehe 7 Januari mwaka huu baada ya kumwangusha John Mahama, rais aliyekuwa madarakani.

Katika hotuba yake aliyoitaoa Rais Addo ameahidi kuinua uchumi wa Ghana kwa kukuza biashara, kuongeza ajira.

Pia ameahidi kutokomeza umaskini katika taifa hilo huku akiwataka raia wa taifa hilo kushirikiana katika kutekeleza azma ya kuleta maendeleo ya taifa hilo.

“Nawaomba tuwe raia ambao sio watazamaji, raia tusiwe wa mameno, wajibu wa raia ni kujenga jamii yake na kuliletea maendeleo taifa lake. Tufanye kazi hadi pale tutakapoona kazi zimekwisha” amesema Rais Addo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Kimataifa

Rais mstaafu ahukumiwa miaka 4 jela

Spread the loveMahakama ya mjini Tunis imemhukumu rais wa zamani wa Tunisia,...

Kimataifa

Malawi yaondoa vikwazo vya viza kwa nchi 79 ikiwamo TZ

Spread the loveWaziri wa usalama wa ndani nchini Malawi, Ken Zikhałe ametangaza...

Kimataifa

Jeshi Kongo lazima jaribio la M23

Spread the loveJeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo jana Jumatano lilizima...

KimataifaTangulizi

Rais wa Namibia amefariki dunia

Spread the loveHAGE Gengob, Rais wa Namibia, amefariki dunia wakati akipokea matibabu...

error: Content is protected !!