Tuesday , 30 May 2023
Home Kitengo Habari Kimataifa Rais abaka, atesa, ashinikiza mauwaji
Kimataifa

Rais abaka, atesa, ashinikiza mauwaji

Spread the love
MWANAJESHI wa zamani wa serikali ya Yahya Jammeh, iliyotawala taifa la Gambia kwa miaka 22, Luteni Malick Jatta, amekiri kufanya mauaji ya wahamiaji 50 kwa amri ya kiongozi huyo. Anaripoti Mwandishi Wetu… (endelea).

Shirika la utagazaji la BBC, linaripoti kuwa wahamiaji hao wanaume, waliuawa kwa madai kuwa kuhofiakutaka kufanya mapinduzi. 

Wahamiaji hao kutoka Afrika Magharibi waliokuwa wanaeleeka Ulaya, walikamatwa na kuuawa baada ya boti walilokuwa wamepanda nchini Senegal, kuishia nchini Gambia.

Luteni Malick Jatta alieleza hayo wakati akitoa ushahidi mbele ya tume ya ukweli na maridhiano (TRRC), inayochunguza maovu yaliotekelzwa chini ya utawala wa Jammeh.

Kabla ya hatua hiyo, Luteni Jatta, amekiri kuhusika katika mauaji ya mwandishi Deyda Hydara mnamo 2004 kwa agizo la kiongozi huyo wa zamani Gambia.

Deyda alikuwa muasisi mwenza na mhariri msimamizi wa gazeti la The Point la nchini humo.

“Nililipwa kiasi cha dola za Marekani 1,000 kutekeleza maujai hayo, licha ya kwamba ni mpaka siku ya pili ndipo nilipogundua kwamba nilikuwa nimemuua Hydara,” ameeleza Luteni Jatta.

Kiongozi huyo aliyeingia madarakani kupitia mapinduzi ya kijeshi ya mwaka 1994, ametorokea nchini Guinea ya Ikweta mwaka 2017 baada ya kushindwa katika uchaguzi.

Yahaya Jammeah aliingia madarakani akiwa na miaka 29 na kwamba mwaka 2013, aliapa kusalia madarakani kwa “mabilioni ya miaka” Mungu akipenda.

Gazeti la the Point, ambako Hydara alikuwa akifanya kazi kabla ya kuuawa mnamo 2004, limeeleza kuwa imechukua miaka 15 kutambua nani aliyemuua mwandishi huyo.

Katika mtandao wake, gazeti hilo limeweka bango tangu wakati huo lililoambatana na swali, “ni nani aliyemuua Deyda Hydara?”

Gazeti hilo halikutoa tamko jingine kuhusu taarifa hii ya sasa. Hydara aliwahi pia kulifanyia kazi na shirika la habari la AFP na waandishi wasiokuwa na mipaka.

Ripoti yake imesema, wahamiaji wa Afrika magharibi waliokiuwa wanaeleeka Ulaya walikamatwa na kuuawa baada ya boti walilokuwa wamepanda nchini Senegal kuishia nchini Gambia.

Naye Fatou Jallow, aliyekuwa malkia wa urembo nchini humo anadai kuwa “alibakwa” na rais huyo wa zamani, 26 Juni 2019. 

Anasema, alitoroka Gambia baada ya kubakwa wakati Jemmah alipokuwa mamlakani na sasa anaishi nchini Canada. 

Ushahidi wake ni miongoni mwa ripoti ya shirika la haki za kibinadamu la Human Rights Watch ambayo inaelezea madai mengine ya ubakaji na unyanyasaji wa kingono uliotekelezwa na bwana Jammeh.

Mtandao wa BBC ulijaribu kuwasiliana na bwana Jemmeh ambaye kwa sasa anaishi mafichoni Equitorila Guinea , kuhusu madai hayo.

Lakini msemaji wa chama chake cha APPR, Ousman Rambo Jatta, alikana madai hayo yaliotolewa na kusema, “sisi kama chama na raia wa Gambia tumechoka na msururu wa madai ambayo yameripotiwa dhidi ya rais wa zamani.”

“Rais huyo wa zamani hana muda wa kujibu uongo na kampeni za kumuharibia jina. Ni mtu anayemuogopa Mungu ambaye anaheshimu sana wanawake wa Gambia,” ameeleza naibu wa kiongozi wa chama hicho cha APPR.

Bi Jallow alitaka kukutana na bwana Jammeh mwenye umri wa miaka 54 mahakamani ili ashtakiwe.

Amesema, “nimejaribu sana kuficha na kufutilia mbali habari hiyo na kuhakikisha kuwa haitakuwa moyoni mwangu. Kwa kweli sikuweza, hivyo basi nikaamua kuzungumza kwa sababu ni wakati wa kusema ukweli na kuhakikisha kuwa Yahya Jammeh anasikia kile alichokitenda.

Alisema, pia yuko tayari kutoa ushahidi mbele ya tume ya haki na maridhiano nchini Gambia TTR ambayo imebuniwa na rais Adama Barrow ambaye alishinda uchaguzi wa mwezi Disemba 2016.

Tume hiyo ya haki na maridhiano inachunguza ukiukaji wa haki za kibinaadamu wakati wa utawala wa miaka 22 wa bwana Jammeh , ikiwemo ripoti za mauaji ya kiholela , ukatili na kukamatwa na kuzuiliwa kiholela.

Akiongea mbele ya Tume hiyo ya maridhiano, Bi Jallow anasema, wakati anakutana na Rais Jammeh alikuwa na umri wa miaka 18. Ilikuwa baada ya kushinda shindano la malkia wa urembo mwaka 2014, katika mji mkuu wa Banjul.

Miezi kadhaa baada ya kupata taji hilo, Bi Jallow anasema, rais hyo wa zamani alijifanya kama mzazi wakati alipokutana naye akimaptia ushauri, zawadi na fedha na kuandaa maji kupelekwa katika nyumba yao ya familia.

Anasema, katika chakula cha jioni kilichoandaliwa na msaidizi wa rais huyo; anasema alimuuliza iwapo wangeoana. Alikataa wazo hilo pamoja na kwamba aliahidiwa zawadi kedekede.

Anasema, msaidizi huyo wa rais baadaye alisisitiza kwamba anafaa kuhudhuria sherehe ya kidini katika Ikulu ya rais kama malkia wa urembo. Hiyo ilikuwa mwezi Juni 2015.

Lakini alipowasili, Bi Jallow anasema, “nilipelekwa katika makao ya kibinfasi ya rais. Rais alikuwa na hasira sana baada ya kukataa kufunga naye ndoa.

“Nilipigwa kofi na kudungwa sindano katika mkono wangu. Alifuta sehemu zake za siri katika uso wangu, akanisukuma nipige magoti na kunifanya vibaya.”

Msichana huyo baadaye anasema, alijifungia nyumbani kwao kwa siku tatu kabla ya kutorokea nchini Senegal.

Alipokuwa mjini Dakra mji mkuu wa Senegal, Bi Jallow alitafuta usaidizi wa mashirika kadhaa ya haki za kibinadaamu. Wiki chache baadaye alipatiwa ulinzi na kupelekwa nchini Canada ambapo amekuwa akiishi tangu wakati huo.

Tume ya TRRC iliundwa kubaini “rekodi ya historia ya hali, sababu na kiwango cha ukiukaji wa haki za binaadamu uliotekelezwa katika kipindi chaJulai 1994 hadi Januari 2017” ambacho Rais Jammeh alikuwa madarakani. 

Daramy anafichua kwamba kilichobainika kutoka kwenye kikao hicho na kinachoendelea kufichuka ni kuchambuliwa gamba la maovu na muamko usiovutia vile kwa tiafa – unaolilazimu kujitathmini kwa mtazamo mpya na pengine mkali.

Shirika la Human Rights Watch (HRW) na Trial International yanasema, bwana Jammeh alikuwa na mfumo wa kunyanayasa wanawake, ambapo wanawake wengine walikua wakilipwa mshahara na serikali na kufanya kazi katika Ikulu kwa jina “wasichana wa itifaki’,’ ambao walikuwa wakifanya kazi za ukarani lakini umuhimu wao mkubwa ulikuwa kushiriki ngono na rais.

Afisa mmoja wa zamani nchini humo ambaye alikubali kuzungunza bila jina lake kufichuliwa anakiri kuwa kuna mambo mabaya yalitendeka katika ofisi ya rais.

Maafisa wa itifaki walikuwa wanawake na waliajiriwa ili kuridhisha mahitaji ya rais. Anakumbuka kumuona Bi Jallow katika Ikulu, wakati mwingine nyakati za usiku.

Mwanamke mwengine ambaye aliajiriwa kama afisa wa itifaki akiwa na umri wa miaka 23 alilazimishwa kushiriki ngoni na bwana Jammeh mwaka 2015.

Mwanamke huyo ambaye aliomba kutofichuliwa jina, alisema kuwa siku moja rais huyo alimwita chumbani mwake. 

“Alianza kunivua nguo na kusema kuwa alikuwa ananipenda, angenifanyia chochote ningetaka na familia yangu, na kwamba nisiambie mtu yeyote na iwapo nitakiuka hilo nitakiona cha mtema kuni.

”Nilihisi sina chaguo. Siku hiyo alilala nami bila kutumia kinga yoyote.”

Mwanamke mwengine ambaye alifanya kazi kama afisa wa itifaki alisema kuwa alijuwa kwamba iwapo mmoja wao angeitwa ingekuwa kwa sababu ya kushiriki ngono.

Wengine walitaka. Walihisi kuheshimiwa ama walitaka pesa, aliambia shirika la haki za kibinadamu la HRW akificha jina lake.

Alielezea vile alivyonyanyaswa kingono na rais huyo nyumbani kwake huko Kanilai, 2013 wakati alipokuwa na umnri wa miaka 22: “Jioni moja msaidizi mmoja wa rais aliniita na kuniambia kwamba na kuandamana naye katika nyumba ya kibinafsi ya rais .

”Alinitaka kuvua nguo. aliniambia kwamba mimi ni msichana mdogo niliyehitaji ulinzi na alitaka kunipaka maji ya kiroho”.

Katika kisa kingine siku iliofuata, alianza kulia wakati bwana Jammeh alipoanza kumshika mwili wake.

Alikasirika na kumfukuza. Anasema kwamba baadaye alifutwa kazi huku ahadi ya kupata ufadhili wa masomo ikifutiliwa mbali.

Rais Barrow amesema kuwa atasubiri ripoti hiyo ya tume ya maridhiano kabla ya kuamua iwapo atamrudisha bwana Jammeh nyumbani kutoka mafichoni nchini Equitorial Guinea.

Lakini Yahya Jammeh ni nani hasa?

Alikuwa Rais wa Gambia. Aliingia madarakani kupitia mapinduzi mnamo 1994 akiwa na miaka 29; na kiongozi ambaye aliamuru mauaji ya wahalifu na wanasiasa wa upinzani walio kwenye hukumu ya kifo.

Mwaka 2008, alionya kuwa wapenzi wa jinsia moja watakatwa vichwa na akakana kuwa majeshi ya usalama yalimuua mwandishi wa habari, Deyda Hydara mnamo mwaka 2004.

Atimuliwa madarakani Januari 2017 kupitia nguvu za kieneo baada ya kushindwa katika uchaguzi 2016.

Mwandishi wa Sierra Leone na Gambian Ade Daramy anasema, raia wa Gambia wanajaribu kupokea maovu yaliotekelezwa wakati wa utawala uliokuwepo.

Lakini anaeleza kwamba kuna kitu ambacho kinawaondolea raia hao wa Gambia tabasamu, vikao vya tume hiyo ya ukweli na maridhiano (TRRC).

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Kimataifa

Mkutano wa Quad Hiroshima waibuka na kutafuta amani na ustawi wa Indo-Pacific

Spread the love  JITIHADA za mazungumzo ya Pande Nne (Quad), hazikuthaminiwa na...

KimataifaTangulizi

Mtuhumiwa wa mauaji ya halaiki ya Rwanda akamatwa Afrika Kusini

Spread the love  MMOJA wa watuhumiwa wakuu wa mauaji ya Kimbari ya...

Kimataifa

Kiwango cha ukosefu wa ajira nchini China chaongezeka

Spread the love  WAKATI kiwango cha ukosefu wa ajira kwa vijana nchini...

Kimataifa

Kampuni za kigeni zahofia kuendelea na biashara China

Spread the love OPERESHENI ya kiuchunguzi inayofanywa na Serikali ya China kwa...

error: Content is protected !!