December 7, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Rais aagiza Kilombero, Ifakara kufanyiwa mabadiliko

Suleiman Jafo, Waziri wa Tamisemi

Spread the love

RAIS John Magufuli amemuelekeza Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Suleman Jafo kufanya mabadiliko kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Ifika na Kilombero mkoani Morogoro. Anaripoti Faki Sosi …(endelea).

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo tarehe 3 Novemba 2019, na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi, kwamba Rais Magufuli amemuagiza Waziri Jafo kubadilisha jina la Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero na kuitwa Mlimba ambapo ameagiza makao makuu yawe Mgeta.

Pia amemwagiza kufanywa mabadiliko kwenye Halmashauri ya Mji Ifika kwa kuziongozea kata kutoka kwenye Halmashauri ya Mji wa Kilombero, na kwamba makao makuu yawe Ifikara Mjini.

error: Content is protected !!