September 29, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Raia wa Rwanda wapandishwa kizimbani Ufaransa

Spread the love

SERIKALI ya Ufaransa imewapandisha mahakama raia wawili wa Rwanda- Octavian Ngenzi na Tito Barahira kwa madai ya kushiriki katika mauaji ya Kimbari yaliyotokea mwaka 1994, anaripoti Wolfram Mwalongo.

Shirika la Utangazaji la Ujerumani (DW) limeeleza kwamba, raia hao wa Rwanda walikuwa mameya katika Mji wa Kabarondo nchini humo kwa vipindi tofauti.

Wanyarwanda hao wanatuhumiwa kuua raia wa Kitusi waliokuwa wamejihifadhi kwenye kanisa tarehe 13 Aprili 1994 nchini humo.

Mahakama ya Rwanda mwaka 2009 iliwahukumu kifungo cha maisha lakini walafanikiwa kukimbilia nchini Ufaransa.

Wakati wa maadhimisho ya miaka 20 ya mauaji ya Kimbari yaliyotokea mwaka 1994, Paul Kagame, Rais wa Rwanda alilaumu vikosi vya Ufaransa kwamba, vilihusika kwenye mauaji hayo yaliyogharimu maisha ya watu zaidi ya 800,000.

Hata hivyo, kuchukuliwa hatua kwa watuhumiwa hao ni mara ya pili baada ya Pascal Simbikangwa ambaye alikuwa kapteni Jeshi la Rwanda kupandishwa kizimbani na hukumiwa miaka 25 jela kwa kuhusika na mauaji hayo.

error: Content is protected !!