Friday , 19 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Raia wa kigeni wanaswa wakitorosha dola 70,000
Habari MchanganyikoTangulizi

Raia wa kigeni wanaswa wakitorosha dola 70,000

Spread the love

RAIA wawili wa kigeni, Nada Zaelnoon Ahamed (38) na Mohamed Belal (31), wanashikiliwa na Jeshi la Polisi baada ya kukutwa na kiasi cha Dola za Kimarekani 70,000 (Sh. 190 milioni), wakitaka kuzisafirisha kwenda nje ya nchi. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Nada Ahamed (38), ni raia kutoka Sudan Kusini na Mohamed Belal (31) anatokea nchini Syria. Wote wawili wamekamatwa kwenye kiwanja cha Ndege cha Kimataifa (JNIA).

Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini, Baranabas Mwakalukwa amesema, watuhumiwa hao wamekamatwa kufuatia kushindwa kutoa taarifa juu ya fedha walizokuwa nazo.

Amesema, kitendo cha kutotoa taarifa ya fedha kwa wasafiri wanaotaka kusafirisha kiasi kikubwa cha fedha, ni kinyume na Sheria ya Utakatishaji Fedha ya mwaka 2006 iliyofanyiwa marekebisho 2012.

Kwa mujibu wa Mwakalukwa, Nada alikuwa anaelekea Nairobi nchini Kenya. Alikuwa anatumia ndege ya Shirika la Kenya Airways na Mohamed alikuwa akielekea nchini Syria. Alikuwa anatumia ndege ya Shirika la Ndege la Ethiopia.

Amesema, Nada ndiye aliyekuwa wa kwanza kukamatwa na fedha hizo, ambapo alikutwa na dola 60,000 na paundi za Sudani 3,410 na kwamba baada ya kubanwa alimtaja mshirika wake Belal aliyenaswa na dola 10,000 (elfu kumi).

Kamanda Mwakalukwa amesema, watuhumiwa hao wamezuiwa na kwamba hawawezi kuendelea na safari zao kwa ajili ya kupisha uchunguzi ili hatua za kisheria zichukuliwe dhidi yao.

Kufuatia tukio hilo, Mkurugenzi wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Richard Mayongela, ametoa wito kwa wasafiri, wadau na watumishi wa mamlaka hiyo na vyombo vya dola kutoa taarifa za vitendo vya kihalifu ili mamlaka stahiki zichukue hatua.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

NEMC yaonya wanaojenga bila tathmini ya mazingira

Spread the loveBARAZA la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC),...

Habari za SiasaTangulizi

Mpina ataka Waziri Majaliwa ajiuzulu, akosoa teuzi za mawaziri

Spread the love  MBUNGE wa Kisesa, Luhaga Mpina, amemtaka Waziri Mkuu, Kassim...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB Pesa Akaunti yawavutia wakaguzi wa ndani Afrika

Spread the loveUbunifu wa bidhaa bora wa Benki ya NMB pamoja na...

KimataifaTangulizi

Mkuu wa majeshi Kenya afariki, Ruto atangaza maombolezo

Spread the loveRais wa Kenya, William Ruto ametangaza maombezo ya siku tatu...

error: Content is protected !!