October 7, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Raia wa Hungary kortini kwa dawa za kulevya

Spread the love

AKOS Berger, Raia wa Hungary amepandishwa kizimbani kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kujibu mashtaka ya kuhujumu uchumi na kukutwa dawa za kulevya. Anaripoti Faki Sosi … (endelea).

Mbele ya Hakimu Mkazi, Maira Kasonde, Groria Mwenda Wakili wa Serikali amemsomea mashtaka moja Berger ya uhujumu uchumi na kukutwa na dawa za kulevya.

Wakili Mwenda amedai kuwa tarehe 19 Julai Mwaka huu akiwa eneo la Mbezi Beach jijini Dar es Salaam, alikuwa akisafirisha dawa za kulevya kilogramu 250 aina ya Psychotropic.

Mshitakiwa huyo hakutakiwa kujibu chochote kutokana na kushitakiwa kwa hati ya uhujumu uchumi.

Mshitakiwa amerejeshwa mahabusu mpaka tarehe 9 Agosti Mwaka huu.

error: Content is protected !!