Wednesday , 29 March 2023
Home Kitengo Habari Kimataifa Raia Pakistan walilia haki siku ya Mshikamano Kashimir
Kimataifa

Raia Pakistan walilia haki siku ya Mshikamano Kashimir

Spread the love

RAIA wa Pakistani waishio nchini Tanzania wameadhimisha siku ya Mshikamano wa Kashmir (Kashmir Solidarity Day) inayoadhimishwa kila mwaka tarehe 5 Februari huku wakiomba watetezi wa haki za binadamu duniani pamoja na jumuiya za umoja wa mataifa kuondosha ukandamazaji unaofanywa kwa serikali ya India ambayo raia wake wanaishi kimabavu katika jimbo la Kashmir. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Balozi wa Pakistani nchini Tanzania, Muhammad Azam Bihan ametoa wito huo kwa kueleza kuwa kinachoendelea katika jimbi la Kashmir ni uonevu dhidi ya raia wa Pakistan.

Balozi Bihan amesema ni muhimu duniani kukawa na usawa kwa kutambua haki za watu wetu.

“Kinachoendelea Kashmir ni uonevu hakipaswi kuungwa mkono na taifa lolote linalothamini haki ya binadamu,” amesema Balozi Bihan.

Balozi huyo amesema ukatili na kuikalia Kashmir kinyume cha sheria ni ukandamizaji wa haki hivyo ameziomba jumuiya za Kimataifa kusimama pamoja na Pakistani.

Balozi Bihan ameviomba vyombo vya habari, wanaharakati wa haki za binadamu na asasi za kiraia kupaza sauti za kutaka Serikali ya India kuacha uchokozi dhidi ya taifa lao.

“Ni miaka 79 sasa nchi yetu ipo njia panda kati ya uhuru na ukandamizaji kwa jirani zetu wahindi kuamua kuikalia ardhi yetu isivyo kisheria” amesema.

India inatawala Bonde la Kashmir lenye idadi kubwa ya watu na jimbo lenye Wahindu wengi karibu na mji wa Jammu, wakati Pakistan inadhibiti sehemu ya mpaka wa upande wa magharibi inayofahamika kama Azad Kashmir. China ina kipande chenye idadi ndogo ya watu katika eneo la nyanda za juu la kaskazini.

Serikali ya New Delhi iliifuta hadhi maalum ya sehemu yake ya Kashmir ya Himalaya inayofahamika kama Jammu na jimbo la Kashmir, tarehe 5 Agosti mwaka jana na kuchukua hatua ya kutuliza ghasia kwa kukata mawasiliano na kuweka vizuizi kwa uhuru wa watu kutembea.

Hatua ya India kufuta hadhi maalum ya majimbo ya Jammu na Kashmir yanazuia.

Jimbo hilo limekuwa likigombaniwa na nchi hizo mbili kwa miaka mingi na Januari mwaka huu, Waziri Mkuu wa India, Narendra Modi alitangaza kuwa raia wa India wanaoishi kwenye jimbo hilo watapiga kura.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Kimataifa

Nyumba ya babu yake Makamu wa Rais wa Marekani yatafutwa Zambia

Spread the love  KAMALA Harris, makamu wa rais wa Marekani, amepanga kutembelea...

Kimataifa

Benki ya Uswizi mbioni kuziwekea vikwazo akaunti za siri za Wachina

Spread the love  WAKATI Serikali na Benki ya Uswizi ikichukua hatua kali...

Kimataifa

Netanyau asitisha mipango yenye utata marekebisho mfumo wa sheria

Spread the love  WAZIRI Mkuu wa nchini Israel, Benjamin Netanyahu amesema atachelewesha...

Kimataifa

Raila ahutubia waandamanaji, mabomu yarindima

Spread the loveMSAFARA wa kiongozi wa Azimio la Umoja-One Kenya, Raila Odinga...

error: Content is protected !!