June 26, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Rage adai jengo la abiria Tabora

Uwanja wa ndege Tabora

Spread the love

MBUNGE wa Tabora Mjini, Ismail Aden Rage (CCM), amehoji mpango wa Serikali wa kujenga jengo la abiria katika uwanja wa ndege mkoani Tabora akitaka kujua utaanza lini. Anaandika Danny Tabason … (endelea).

“Mheshimiwa mwenyekiti, mkoa wa Tabora tulipewa ahadi na serikali ya kujenga jengo la abiria katika uwanja wa ndege. Nataka kujua kama mpango huo upo na lini ujenzi huo utaanza? Amehoji.

Katika majibu ya serikali, Naibu Waziri wa Uchukuzi, Dk. Chalres Tizeba, amekiri kwamba wanao mpango huo ambapo hivi sasa zabuni imeshatangazwa.

“Hivi sasa inafanyika tathmini ambayo itapelekwa Benki ya Dunia kwa ajili ya kuanza ujenzi wa jengo hilo na fedha zake zipo,”amesema Dk.Tizeba.

Aidha, katika jibu la swali la mbunge wa Viti Maalum, Felister Bura (CCM), aliyetaka kujua ni lini serikali itaanza ujenzi wa uwanja wa ndege katika eneo la Msalato mkaoni Dodoma, Dk. Tizeba ameliambia Bunge kuwa, mchakato wa  ujenzi wa uwanja huo upo katika hatua nzuri ya mazungumzo na wawekezaji.

Awali katika swali la msingi, Mbunge wa Kishapu, Suleiman Nchami (CCM), alitaka kujua lini serikali itajenga uwanja wa ndege katika wilaya ya Kishapu.

error: Content is protected !!