July 1, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Radi yaua wanafunzi saba na mwalimu

Mwalimu Veronika Mtesi akiwa hospitali

Mwalimu Veronika Mtesi wa shule ya msingi Kibirizi aliyepata mshtuko baada ya tukio la radi akiwa katika hospitali ya Mawenzi mkoa wa Kigoma kwa matibabu

Spread the love

WANAFUNZI sita wa darasa la kwanza katika Shule ya Msingi Kibirizi eneo la Bangwe, Halmashauri ya Manispaa ya Mji wa Kigoma pamoja na mwalimu wao, ni miongoni mwa watu wanane waliofariki huku wengine watano wakijeruhiwa kwa kupigwa na radi. Anaandika Pendo Omary … (endelea).

Akizungumza na MwanaHALISI Online kwa simu, ACP Jafary Mohamed- Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kigoma, amesema “katika tukio hili wanafunzi sita wamekufa. Wasichana ni watatu na wavulana ni watatu. Pia mwalimu mmoja wa kike na raia mmoja.”

“Tukio hili limetokea saa 5:45 leo asubuhi. Wanafunzi hao walikuwa darasani huku mwalimu akiwa ofsini kwake. Wote ni wa shule ya msingi Kibirizi. Maiti hao wamehifadhiwa katika Hospitali ya Mkoa ya Maweni,” amesema Mohamed.

Aidha, Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Maweni, Fadhili Kabaya amenukuliwa na vyombo vya habari akisema awali majeruhi walikuwa 15. Baada ya matibabu, majeruhi 10 wameruhusiwa na watano wakiwa bado wamelazwa.

Kabaya ametaja majina ya waliokufa kuwa ni Yusuph Ntahoma (8), Hassan Ally (9), Fatuma Sley (7), Zamda Seif (8), Shukranmi Yohana (7) na Harupe Kapupa (10).

Wengine ni Mwalimu Elinaza Mbwambo (25) na Forcus Ntahaba (45) mkazi wa eneo la Bangwe.

Radi hiyo imeambatana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha nchini ukiwemo mkoa wa Kigoma huku Mamla ya Hali ya Hewa ikiwa imetoa tahadhari kuwa “mvua zitaendelea kunyesha hadi mwezi wa tano”.

error: Content is protected !!