May 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

R. Kelly majanga, akutwa na hatia

Spread the love

 

MWANAMUZIKI nguli wa miondoko ya ‘RnB’ kutoka nchini Marekani, Robert Sylvester Kelly maarufu kama R. Kelly amekutwa na hatia katika tuhuma zilizokuwa zikimkabili za kuwanyanyasa wanawake na watoto kingono. Anaripoti Matilda Buguye…. (endelea).

R. Kelly amekutwa na hatia hiyo tarehe 27 September, 2021 baada ya walalamikaji 11 kati yao wanawake tisa na wanaume wawili kutoa ushuhuda wao kizimbani.

Mbali na tuhum za ngono, R.Kelly pia alikuwa akituhumiwa kwa rushwa, utekaji pamoja na kufanya biashara haramu ya binadamu ambako katika makosa yote msanii hiyo amekutwa na hatia.

Pia anadaiwa kutumia umaarufu wake na utajiri wake kuwarubuni wanawake na watoto kwa ahadi za kuwasaidia kimuziki.

Hukumu ya msanii R. Kelly inatarajiwa kutolewa tarehe 4 Mei mwaka 2022 na huenda akahukumiwa kifungo kisichopungua miaka 20 jela au kifungo cha maisha.

R. Kelly aliwahi kuipagawisha dunia kwa namna ya uimbaji wake na kipaji chake kilichobarikiwa miaka hiyo ya 90 kiasi cha kuitwa ‘Mfalme wa Rnb’ kwa nyimbo zake kali kama; I believe i can fly, Stormy is over, Gotham city, Bump n grind na nyingine kibao ambazo hata sasa mashabiki wake bado wanazikubali

error: Content is protected !!