Saturday , 20 April 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Puto la Kijasusi la China latia mashaka mahusiano yake na Marekani
Kimataifa

Puto la Kijasusi la China latia mashaka mahusiano yake na Marekani

Spread the love

 

PUTO la Kijajasusi la China liliorushwa kwenye anga ya Marekani limetajwa kuwa chanzo cha kuteteresha mahusiano ya nchini hizo mbili. Imeripoti Mitandao ya Kimataifa … (endelea).

Puto limeibua maswali kuhusu shughuli za Jeshi la Ukombozi la Watu wa China (PLA), hesabu za hatari za Mwenyekiti Xi Jinping, viwango vya mawasiliano kati ya PLA na Wizara ya Mambo ya Nje ya China (MFA) na kwa nini China inaeleza puto hilo kuzunguka angahewa ya dunia.

Hakuna shaka yoyote kuwa puto hili ni la kichina na kwamba serikali ya Marekani imeweka hadharani kuguswa na urushwaji wa puto hilo.

Maafisa wa ulinzi pia walifichua Jumamosi kwamba puto hilo liliingia kwenye anga ya Marekani tarehe 28 Januari karibu na Visiwa vya Aleutian, kabla ya kuhamia anga ya Canada siku tatu baadaye na kuingia tena Marekani tarehe 31 Januari. kitu hicho kilionekana katika jimbo la Montana nchini Marekani, ambalo ni nyumbani kwa maeneo kadhaa nyeti ya makombora ya nyuklia.

Uhusiano kati ya China na Marekani umeathiriwa na tukio hilo, huku Pentagon ikilitaja kuwa “ukiukwaji usiokubalika” wa uhuru wa Marekani.

Blinken, mwanadiplomasia mkuu wa Marekani – aliiambia Beijing, kitendo cha kutowajibika kabla ya safari yake ambayo sasa imeahirishwa ingekuwa mkutano wa kwanza wa ngazi ya juu kama huo wa Marekani na China kwa miaka mingi.

Lakini China ulitaka kuahirisha ziara yake, ikisema katika taarifa yake Jumamosi kwamba hakuna upande uliotangaza rasmi mpango wa safari.

Wizara ya Mambo ya Nje ya China ilisema Beijing haitakubali dhana yoyote isiyo na msingi au porojo na ikashutumu baadhi ya wanasiasa na vyombo vya habari nchini Marekani kwa kutumia tukio hilo kama kisingizio cha kushambulia na kuipaka matope China.

Pentagon ilisema puto ya pili ya kijasusi ya Uchina imeonekana – wakati huu katika eneo la Amerika ya Kusini na kuripotiwa kuonekana juu ya Costa Rica na Venezuela.

Jeshi la wanahewa la Colombia linasema kitu kilichotambuliwa kinachoaminika kuwa puto kiligunduliwa mnamo 3 Februari katika anga ya nchi hiyo kwa zaidi ya futi 55,000.

Inasema ilifuata kitu hicho hadi ilipoondoka kwenye anga na kuongeza kuwa haikuwakilisha tishio kwa usalama wa taifa.

China bado haijatoa taarifa yoyote hadharani kuhusu puto ya pili iliyoripotiwa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

KimataifaTangulizi

Mkuu wa majeshi Kenya afariki, Ruto atangaza maombolezo

Spread the loveRais wa Kenya, William Ruto ametangaza maombezo ya siku tatu...

Kimataifa

Majaji kuamua hatima ya Zuma leo

Spread the loveMajaji nchini Afrika Kusini leo Jumanne wataamua ikiwa rais wa...

Habari za SiasaKimataifa

Spika Afrika Kusini ajiuzulu kwa tuhuma za rushwa

Spread the loveSpika wa Bunge la Afrika Kusini, Nosiviwe Mapisa-Nqakula ametangaza kujiuzulu...

Habari MchanganyikoKimataifa

Tetemeko la ardhi laua 7, lajeruhi 800 Taiwan

Spread the loveWatu wapatao saba wamefariki dunia na wengine zaidi ya 800...

error: Content is protected !!