RAIS wa Urusi, Vladimir Putin jana tarehe 27 Disemba, 2022 amesaini amri ambayo inaweka marufuku ya uuzaji wa mafuta na bidhaa za mafuta kwa mataifa yaliyoweka kikomo cha bei ya mafuta ya Urusi kuanzia tarehe 1 Februari 2023 kwa kipindi cha miezi mitano. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa … (endelea).
Kundi la G7 la nchi tajiri duniani, Umoja wa Ulaya na Australia walikubaliana mwezi huu kuweka kikomo cha dola 60 kwa pipa moja la mafuta ghafi ya Urusi, hatua ambayo ilianza kutekelezwa tarehe 5 Disemba 2022 kwa sababu ya operesheni maalum ya kijeshi ya Moscow nchini Ukraine.
Amri hiyo ya Urusi ilieleza kiwa hatua hiyo inaanza kutekelezwa tarehe 1 Februari, 2023, na inaendelea hadi tarehe 1 Julai, 2023.”
Leave a comment