August 10, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Putin akoleza mahaba kwa Trump

Vladimir Putin, Rais wa Urusi

Spread the love

VLADIMIR Putin, rais wa Urusi amemwandikia barua ya kumtakia heri ya sikuu ya krismasi na mwaka mpya Donald Trump ambaye ni rais mteule wa Marekani anayetarajiwa kuapishwa tarehe 20 Januari mwakani, anaandika Wolfram Mwalongo.

Katika barua hiyo, Rais Putin ameeleza kuwa azma yake ni kuimarisha mahusiano huku suala la muhimu ni kuimarisha ulinzi baina ya mataifa hayo na kudaikuwa ana imani kubwa na Rais Trump akiamini atafanya mengi yatakayosaidia Urusi na Marekani kusonga mbele zaidi.

Haya yanajiri ikiwa ni siku moja tu tangu Trump aweke wazi azma yake ya kuimarisha silaha za nyuklia kutokana na mataifa makubwa kushindwa kutoa msimo wa kudhibit silaha hizo huku Rais Putin pia akionekana kujikita katika utengenezaji wa silaha hizo.

Wachambuzi wa masuala ya kisiasa wanasema ukaribu unaoneshwa na Putin kwa Trump una walakini hususan wakati huu ambao mataifa hayo yanaendelea kusigana katika kuresha hali ya amani nchini Syria.

Aidha, shutuma zinazoelekezwa  kwa Urusi na Shirika la Ujasusi la Marekani (CIA), pamoja na lile la upelelezi (FBI) kwamba Urusi imehusika moja kwa moja katika njama za kufanikisha ushindi wa Trump katika uchaguzi kuu wa tarehe 11 Novemba  mwaka huu.

Chama cha Democratic pia kinalalamikia udukuzi uliofanywa kwenye kompyuta za mgombea wake Hillary Clinton, aliyekuwa Waziri  Mambo ya Nje wa zamani wa taifa hilo ambapo udukuzi huo ulifanikiwa kutoa mambo ya siri ya mgombea huyo muda mfupi kabla ya uchaguzi mkuu.

error: Content is protected !!