Thursday , 25 April 2024
Home Habari Mchanganyiko PURA yaanzisha kanzidata
Habari Mchanganyiko

PURA yaanzisha kanzidata

Spread the love

 

MAMLAKA ya Udhibiti Mkondo wa Juu wa Petroli nchini Tanzania (PURA), imeanzisha Kanzidata (CQS) ambayo itawezesha kampuni na mtu mmoja mmoja kujisajili na kushiriki mchakato wa utafutaji na uchimbaji wa mafuta nchini. Anaripoti Selemani Msuya, Dar es Salaam … (endelea).

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Kitengo cha Ushiriki wa Wazawa na Ushirikishwaji wa Wadau PURA, Charles Nyangi wakati akizungumza na waandishi wa habari katika Maonyesho ya Biashara ya Kimataifa ya 46 maarufu Sabasaba yanayofanyika katika Kiwanja cha Mwalimu Julius Nyerere Temeke Dar es Salaam.

Amesema PURA wameshiriki maonesho hayo ya 46 kwa lengo la kutoa elimu kuhusu fursa zinazopatina nchini katika eneo la gesi na mafuta.

Nyangi amesema Kanzi Data hiyo itawezesha kila mtu anayetaka kushiriki katika eneo hilo la utafutaji na uchimbaji wa gesi kupata taarifa mbalimbali zinazowekwa na PURA.

“PURA imedhamiria kuvutia wawekezaji wa ndani na nje ya nchi hasa wa ndani, tumeanzisha Kanzi Data ambayo wazawa kupitia makampuni yao kujisajili ambapo kila kitu ambacho kitahitajika kwa mwekezaji kinakuwepo kwenye CQS hiyo.

Mfano ili kupewa kazi katika eneo hilo la utafutaji na uchimbaji wa mafuta unatakiwa kuwasilisha nyaraka mbalimbali kama leseni, cheti ya kulipa kodi, kuandaa mahesabu na vingine, hivyo kwa sasa watakuwa wanaweka hapo na ikitokea kazi inakuwa rahisi kuwapigania,” amesema.

Mkuu huyo wa kitengo alisema PURA inaendelea kutoa elimu ya umuhimu wa wazawa kushiriki katika kazi za uchambaji, ununuzi, ukaratabati na nyingine ambazo zinafanyika katika eneo hilo.

Nyangi amesema kutokana na hamasa hiyo ambayo wamekuwa wakitoa kwa wazawa, hadi sasa kampuni tatu zimefanikiwa kupata zabuni katika kampuni za uchimbaji na utafutaji wa mafuta na gesi.

Amesema baadhi ya kampuni zimepata zabuni za kufanyia ukarabati wa visima vya Kampuni ya Songo Songo ambapo zimeingiza zaidi ya Sh.bilioni 2.

Aidha, Nyangi ametoa wito kwa Watanzania kushiriki kikamilifu wakati wa Mradi wa Kuzalisha Gesi wa LNG ukianza, ambao mkataba wa awali umeshasaini kati ya Serikali na wawekezaji na zaidi ya Sh.trilioni 70 zinatarajiwa kuwekezwa.

Amesema PURA inaendelea kutoa elimu kwa jamii na Watanzania wote kuendelea kushiriki katika shughuli mbalimbali ambazo zitahitaji kada ya aina yoyote, kama vibarua au ajira za kudumu.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Majaliwa: Mvua zimesababisha vifo vya watu 155, kuendelea hadi Mei

Spread the love  WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amesema mvua kubwa za El-Nino...

Habari Mchanganyiko

Exim Bank yatoa  vitanda kwa shule ya Jeshi la Polisi Moshi

Spread the love  BENKI ya Exim imekabidhii  seti ya vitanda kwa Shule...

Habari Mchanganyiko

NBC yakabidhi vitanda Shule ya Polisi Moshi

Spread the loveBenki ya NBC imekabidhi msaada wa vitanda 28 kwa Shule...

Habari Mchanganyiko

THRDC yaongeza mkataba wa ushirikiano na ABA

Spread the love  MTANDAO wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC),...

error: Content is protected !!