May 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Ruud Van Nistelrooy aula PSV Eindhoven

Spread the love

MSHAMBULIAJI, wa zamani wa Manchester United, Ruud Van Nistelroy ameteuliwa kuwa kocha Mkuu wa Klabu ya PSV Eidhoven inayoshiriki Ligi Kuu nchini Uholanzi.

Kiungo huyo wa zamani mwenye umri wa miaka 45 ambaye pia ni raia wa Uholanzi   atachukua nafasi ya Roger Schmidt ambaye   ataondoka mwishoni mwa msimu huu, baada ya mkataba wake utakapomalizika. Anaripoti Rhoda Kanuti… (endelea).

Nahodha huyo alifanikiwa kufunga mabao 62 katika mechi 67 alizocheza akiwa PSV mwaka 1998 hadi mwaka 2001, kabla ya ya kuwa na miaka mitano yenye mafanikio zaidi akiwa Manchester United.

Van Nistelrooy alitwaa Kombe la FA na Kombe la Ligi enzi huko Uingereza, kisha kushinda taji la ligi kuu Hispania mara mbili slipohamia Real Madrid.

Amesema kwamba siku zote imekuwa ndoto yake kuwa Kocha Mkuu wa PSV.

Hata hivyo, alistaafu kucheza mwaka 2012, lakini alikuwa Msimamizi misimu miwili kama Kocha msaidizi wa Timu ya Taifa ya Uholanzi, pia amekuwa akisimamia Timu za Vijana na wachezaji wa akiba wa PSV.

error: Content is protected !!