August 8, 2022

Uhuru hauna Mipaka

PSPF hoi, yapata hasara Sh. 11.6 trilioni

Spread the love

MFUKO wa Pensheni wa PSPF umepata hasara ya Sh. 11.6 trioni huku msingi wa hasara hiyo ikiwa ni serikali kuchelewa kulipa madeni ya mafao ya wanachama waliokuwepo kabla ya kuanzishwa kwa mfuko huo Julai, mwaka 1999, anaandika Dany Tibason.

Wakati hali ikiwa hivyo, Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikari (PAC) imeitaka serikali kuchukua hatua za haraka za kuiokoa PSPF kutokana na kuzidi kuwa na hali mbaya kifedha huku serikali ikiwa ni chanzo.

PAC ilibaini kuwa pamoja na PSPF kupokea michango ya wanachama wake inayofikia Sh. 661 bilioni kwa mwaka lakini hulazimika kulipa mafao yanayofikia Sh. 663 bilioni kwa mwaka na hivyo kuwa na upungufu ya ulipajiwa deni hilo kwa kiasi cha Sh. 2 bilioni.

“Kwa ukaguzi uliofanyika mwaka 2010 walikuwa na hasara ya Sh. 6.2 trilioni lakini mwaka wa fedha 2014/2015 hasara imekua Sh. 11.6 trilioni. Kwa kifupi hatua za haraka zisipochukuliwa mfuko huu unaelekea kufa,” amesema JaphetHasunga, Mbunge wa Jimbo la Vwawa (CCM).

Joseph Kakunda, Mbunge wa Sikonge (CCM) amesema kwa mujibu wa ripoti ya CAG pamoja na deni hilo, la mafao ya wastaafu wa mwaka 1999 pekee mfuko huo una madai ya mikopo kutoka taasisi za serikali yenye thamani ya Sh. 499.7 bilioni.

Akijibu hoja hizo Bi. Doroth Mwanyika, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango amesema serikali itahakikisha madeni yote yanaanza kulipwa hivi karibuni.

“Naihakikishia PAC kuwa hadi kufikia Februari mwakani (2017) madeni haya yote tutakuwa tumeyamaliza, serikali itaanza kulipa deni hilo la mafao kupitia njia ya hati fungani,” amesisitiza.

error: Content is protected !!