Monday , 5 June 2023
Home Kitengo Michezo PSG hatihati kutetea ubingwa Ufaransa
Michezo

PSG hatihati kutetea ubingwa Ufaransa

Spread the love

 

HUENDA kocha Mauricio Pochettino wa kikosi cha PSG, akawa kwenye wakati mgumu wa kutetea taji lake la Ligu Kuu Ufaransa baada ya kuwa nyuma kwa pointi moja nyuma ya Lille wanaongoza ligi hiyo, huku ukiwa umesalia mchezo mmoja. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).

Ligi hiyo ambayo itamalizika mwisho wa wiki hii, huku klabu ya Lille huenda ikavunja ufalme wa PSG kwa kutwaa kombe hilo kama ikishinda mchezo wake wa mwisho.

Kwa sasa Lille wanapointi 80 na michezo 37, baada ya kupata suluhu kwenye mchezo wa jana dhidi ya St-Ettienne, wakati PSG wakishika nafasi ya pili wakiwa na pointi 79 na michezo 38, baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 4-0, mbele ya Reims.

Mauricio Pochettino, Kocha wa PSG

Kwenye michezo ijayo ya mwisho PSG atakuwa ugenini kumenyana na Brest inayoshika nafasi ya 16, kwenye msimamo, huku Lille wakiwa na matumaini makubwa ya ubingwa nao watakuwa ugenini kukipiga na Angers inayoshika nafasi ya 12 kwenye msimamo.

PSG kwa sasa ndiyo bingwa mtetezi wa taji hilo ambalo amelitwaa mara ya tatu mfululizo na kuweka rekodi ya kulichukua mara saba katika kipindi cha miaka 10.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

Samia aipongeza klabu ya Yanga kwa hatua iliyofikia

Spread the love RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia...

Michezo

Yanga waitwa Ikulu kesho Jumatatu

Spread the love RAIS wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, kesho Jumatatu, tarehe...

Michezo

Dk. Mkwizu: Afrika tudumishe utamaduni

Spread the love  MWENYEKITI wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Mkoa wa...

Michezo

‘EONII’ kuteka tasnia ya filamu

Spread the love  UZINDUZI wa Filamu ya Kisayansi ya ‘EONII’ uliofanyika Mei...

error: Content is protected !!