January 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Profesa Ngowi: Bajeti ya Serikali haitekelezeki

Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Mzumbe Profesa Honest Ngowi

Spread the love

MHADHIRI wa Chuo Kikuu cha Mzumbe Profesa Honest Ngowi amesema anawasiwasi kuwa, bajeti ya serikali  2015/16  iliyopitishwa kwa kishindo bungeni haitatekelezeka. Anaandika Jimmy Mfuru … (endelea).

Aidha, Ngowi amesema itakuwa ngumu kuzipata trilioni 22 zilizopitishwa na bunge kwa kuwa ni changamoto kubwa na hazipelekwa kwenye maeneo husika kwa wakati.

Ngowi  ambae ni mtaalamu wa mambo ya uchumi alikuwa akielezea utekelezaji wa bajeti hiyo baada ya kupitishwa kwa zaidi ya asilimia 80.

“Mimi nina wasiwasi na utekelezaji wa bajeti na hizo fedha zinauhakika kama zinapatikana na kuelekezwa kwenye maeneo zilikoelekezwa bado ni changamoto kubwa kwa serikali,” amesema Ngowi.

Licha ya Ngowi sehemu kubwa ya malalamiko kwa baadhi ya wabunge yaliitaka serikali kuangalia upya uamuzi wa kungeza kodi kwenye Mafuta ya Taa, Dizeli pamoja na Petroli.

Hata hivyo, Waziri wa Fedha, Saada Mkuya amesema kuwa, ni lazima wananchi watoe fedha hiyo ili kurahisisha huduma ya umeme kusambaa vijijini.

Akizungumzia lalalamiko ya wabunge kuhusu ongezeko la tozo ya Mafuta ya Taa, Petrol na Dizel amesema, hakuna jinsi ya kukwepa tozo hiyo.

“Hatuwezi kuikwepa tozo hiyo kwani tunahitaji Sh.100 kwa kila lita moja na fedha hiyo ikikusanywa zinaweza kupatikana Sh. bilioni 276 kutokana na tozo ya mafuta kwa kila lita,” amesema Mkuya

error: Content is protected !!