Monday , 4 March 2024
Home Habari Mchanganyiko Profesa Maghembe atoa neno Morogoro
Habari Mchanganyiko

Profesa Maghembe atoa neno Morogoro

Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe
Spread the love

WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe amewahimiza viongozi kuanzia ngazi ya mkoa, wilaya hadi vijiji kuhakikisha wanasimamia uwepo wa bei nzuri ya mazao ya mkulima kulingana na bei ya mazao ya dunia ili kufanya kilimo kuwa na tija na kufikia azma ya maendeleo ya viwanda nchini, anaandika Christina Haule.

Waziri Magembe aliyasema hayo kwenye ufunguzi wa maonesho ya Kilimo, mifugo na Uvuvi na sherehe za Nanenane kanda ya mashariki yaliyofanyika kwenye viwanja vya mwalimu Julius Nyerere mkoani Morogoro.

Prof. Maghembe alisema, ili serikali na nchi kwa ujumla iweze kufikia malengo ya kuwa na uchumi wa kati ikiwemo kuimarisha maendeleo ya viwanda suala la masoko ya uhakika ya mazao halina budi kuzingatiwa kufuatia asilimia 90 ya mazao kutegemewa katika viwanda kama malighafi viwandani.

Amesema, ni muhimu soko la mazao lianzishwe mara moja na kufanya kuondoa bei holela za mazao sambamba na kusimamia ubora wa vifungashio na kuondoa masuala ya Rumbesa.

“Hatuwezi kufikia Taifa la kati huku tukiwa tumebeba wakulima zaidi ya mil 33 bila kuwa na bei stahiki ya mazao, huku ukitaka kuwa na uchumi wa kati” alisema Prof. Maghembe.

Aidha, aliwataka wakulima kusimamia na kufuata maelekezo ya wataalamu wa kilimo kwa kufuata misingi ya sayansi katika kilimo na kuona manufaa ya kilimo.

Amesema kilimo cha kisasa cha kutumia teknolojia na sayansi ya hali ya juu kinapaswa kutumika na kuachana na dhana ya kwenda taratibu katika kilimo kama ilivyo kwa sasa kwa watanzania na wakulima kujikuta hawapigi hatua siku hadi siku.

Hivyo aliwataka wakulima katika miaka 8 iliyobaki kutimiza malengo ya serikali ya kuwa na uchumi wa kati hapo 2025 kuhakikisha wanatumia mazao ya mbegu za GMO ili kuongeza uzalishaji katika mazao.

Pamba ya kawaida inayolimwa Tanzania huzalisha kg 350 kwa heka moja huku pamba ya GMO huzalisha kg 2000 kwa heka moja na kufanya mkulima wa GMO kupata faida kubwa ya mazao na kukua kiuchumi tofauti na wa kawaida, tuache kujivunga na ujima wa kizamani na kutumia mambo ya kisasa” alisema Prof, Maghembe.

Prof. Mghembe alisema kuwa lengo la Serikali ya Tanzania ni kufanya nchi kufikia uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025 na kwamba watanzania wawe na mapato yanayozidi dola za kimarekani 1500 kwenye miaka 8 ijayo kuanzia sasa kama walivyokubaliana kupitia ilani ya Chama Cha Mapinduzi na msukumo wa Rais John Magufuli.

Naye Mkuu wa mkoa wa Morogoro Dk. Kebwe Steven Kebwe aliwataka waliouziwa viwanja na kuvikodisha kwa ajili ya shughuli tofauti na maonesho katika uwanja huo kuchukua uamuzi wa kuondoka wenyewe mapema kabla hawajapewa notisi ya miezi mitatu kupisha maonesho hayo katika viwanja hivyo.

Dk. Kebwe amesema, Chama cha Wakulima (TASO) kiliamua wakodisha watu kwa ajili ya makazi na biashara tofauti na makusudio ya maonesho jambo ambalo halileti maana ya maonesho na kwamba vikao vya kamati kupitia TAMISEMI wameamua kutoa notisi kwa wakazi hao ili wapishe maeneo hayo.

Amesema, uwanja huo ulitengwa mahususi kwa ajili ya maonesho ya kilimo, uvuvi na mifugo na kwamba kufanya shughuli nyingine tofauti hakutawezesha dhima ya elimu iliyokusudiwa kuweza kuwafikia wakulima.

Awali Katibu tawala wa mkoa wa Morogoro, Cliford Tandari alisema, baada ya maonesho hayo kurudishwa kwao kama TAMISEMI wameweza kuongeza makusanyo hadi kufikia mil 80 kwa sasa na wanaweza kufikia mil 140 baada ya maonesho kuisha na kwamba fedha hizo zinaweza kuwasaidia kutatua changamoto katika uwanja huo ikiwemo uchache wa maji, ukosefu wa uzio na kuboresha uwanja kuwa na maonesho ya kudumu.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

TEF yaomboleza kifo cha Mzee Mwinyi

Spread the loveJukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) limeeleza kupokea kwa masikitiko taarifa...

AfyaHabari Mchanganyiko

Maambukizi ya UKIMWI Lindi yapungua

Spread the loveMaambukizi ya Virusi vya UKIMWI yamepungua katika Manispaa ya Mkoa...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mgomo kitita kipya cha NHIF: Serikali yaita hopsitali binafsi mezani

Spread the loveSERIKALI imekiita mezani Chama cha Wenye Hospitali Binafsi (APHFTA), ili...

Habari Mchanganyiko

Karafuu, Parachichi yawa fursa Morogoro

Spread the loveIMEELEZWA kuwa zao la karafuu ambalo kwa sasa linalimwa pia...

error: Content is protected !!