Sunday , 3 December 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Profesa Lipumba kugombea urais Tanzania
Habari za Siasa

Profesa Lipumba kugombea urais Tanzania

Spread the love

TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), imemteua Profesa Ibrahim Lipumba kuwa mgombea urais wa Tanzania kupitia Chama Cha Wananchi (CUF) na mgombea mwenza, Hamida Abdallah Huweishi katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Jumatano 28 Oktoba 2020. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma…(endelea).

Profesa Lipumba ni mgombea wa saba kuteuliwa na Mwenyekiti wa NEC, Jaji Semistocles Kaijage leo Jumanne tarehe 25 Agosti 2020 ofisi za tume hiyo jijini Dodoma.

Pia, Philip John Fumbo wa chama cha DP ameteuliwa na NEC kugombea urais kwenye uchaguzi huo. Fumbo na mgombea wake mwenza, Zainabu Juma Khamisi wamekuwa wagombea wa nane kuteuliwa.

 

Vyama vilivyojitosa kuchukua fomu vilikuwa 17 kati ya 19 vilivyochukua fomu. Vyama ambavyo havikuchukua fomu kwenye nafasi hiyo ni TLP na UDP ambavyo vilitangaza kumuunga mkono mgombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais John Pombe Magufuli.

Shughuli ya urejeshaji fomu itahitimishwa saa 10 jioni.

Endelea kufuatilia MwanaHALISI Online, MwanaHALISI TV na mitandao yetu ya kijamii kwa taarifa na habari mbalimbali

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Dk. Biteko aagiza wakurugenzi TANESCO kukemea rushwa kwenye maeneo yao

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Uongozi wa Samia kuendelea hadi 2030

Spread the loveKWETU sisi tuliowahi kusoma sekondari, iwe O levo au A...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Bado askari wastaafu wanaonewa

Spread the loveRAIS wangu Samia Suluhu Hassan tunaendelea kumshukuru Mungu kwamba wote...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Tunastawisha ufisadi na kuchukia matunda yake

Spread the loveBUNGE la Jamhuri linaloendelea mjini Dodoma, kwa wiki nzima limetawaliwa...

error: Content is protected !!