July 6, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Profesa Kahigi apeta Bukombe

Mbunge wa Bukombe (Chadema), Profesa Kulikoyela Kahigi (katikati) akiwa katika ziara jimboni kwake

Spread the love

MBUNGE wa Bukombe (Chadema), Profesa Kulikoyela Kahigi ameibuka kidedea katika kura za maoni kwa kupata 196 huku mpinzani wake Renatus Nzemo aliepata na kura 65. Anaandika Dany Tibason, Dodoma … (endelea).

Katika kinyang’anyiro hicho ambacho kiliwakutanisha makada wa Cahdema wapatao wanne aliyefuatia kwa kura ni Dk.Joseph Mugasa aliyepata kura 7 huku Dk.Julias Mwita akiambulia kura 7.

Uchaguzi huo ambao ulionekana kuwa na upinzania mkali na kupelekea kumalizika saa tano za usiku huku makundi yakionekana kutawala huku baadhi ya wagombea wakitiliwa shaka kuwa ni mamluki wa CCM.

Kwa upande wake Profesa Kahigi muda mfupi baada ya kutangaza matokea alisema hakuna sababu yoyote ya kufanya makundi ndani ya chama.

“Nilazima kuhakikisha tunajenga chama imara kwa misindi ya kuiondoa CCM madarakani ili kuweka mfumo ambayo utakuwa na manufaa kwa jamii nzima.

“Uchaguzi umeisha sasa umefika wakati wa kujenga chama na kuhakikisha ushindi unapatikana tena ushindi wa kishindo, tukigawanyika sisi kwa sisi ni wazi tutakuwa tukitoa nafasi kubwa kwa wapinzania wetu ambao ni CCM” amesema Profesa Kahigi.

Mbali na hilo aliwataka vijana pamoja na wale ambao wanakuwa na sura mbili katika chama kujiepusha na mambo ambayo yanaweza kusababisha kushindwa ndani ya chama.

“Ndugu zangu vijana naomba sana msikubali kutumiwa na wana CCM kwa kuwapatia kitu chochote kwa kwa maana ya kuwashawishi ili kusaliti chama chenu cha matumaini cha Chadema.

“Nyinyi wenyewe ni mashahidi chama kinakuwa asubuhi na jioni lakini siyo kwamba kuimarika kwa chama kunawavutia maadui wetu ambao ni wafuasi wa CCM wanaomba sana tuparanganyike ili waendelee kuwadhulumu na kuwafisadi watanzania ili kuendeleza umasikini ambao umekithiri ” amesema

Naye msimamizi wa Uchaguzi Crispiani Kagoma amesema uchaguzi uliofanyika ni wa awali lakini kazi kubwa itafanywa na Kamati Kuu kwa ajili ya kuteua jina ambalo linafaa na lina vigezo.

Amesema uchaguzi wa kura za maoni usiwe chanzo cha kuwagawa wanachama na badala yake wanatakiwa kuungana ili kuhakikisha wanajenga chama kwa ushirikiano mkubwa ili kukipatia ushindi wa kishindo wakati wa uchaguzi mkuu wa Oktoba 25 mwaka huu.

error: Content is protected !!