October 2, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Profesa Kabudi: Ukiteuliwa na Rais Magufuli usitamani kazi nyingine

Prof. Palamaganda Kabudi, Waziri wa katiba na Sheria

Spread the love

PROFESA Palamaganda Kabudi, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, amewataka watumishi wa umma nchini kuwa waadilifu na uaminifu wakiwa kwenye majukumu yao. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Kabudi amesema hayo leo Jumatatu tarehe 6 Julai 2020  Ikulu ya Chamwino jijini Dodoma kwenye hafla ya Rais John Pombe Magufuli kuapisha viongozi mbalimbali aliowateua hivi karibuni.

Kabudi amesema vyeo walivyopewa ni dhamana yenye thamani mbele ya Mwenyezi Mungu.

“Sisi sote ambao tumepewa dhamana kubwa ya kuwaongoza Watanzania, tujue hakuna kazi ya thamani kubwa machoni mwa Mwenyezimungu kama kuwahudumiwa waja na watu wake,” amesema Profesa Kabudi.

Ametaka wateule hao kuwa waaminifu na wajiepushe kutamani masuala ya kando ya majukumu yao.

Rais John Magufuli

“Tutunze viapo vyetu, tutunze uaminifu wetu na tujue kazi yoyote tunayopewa na mheshimiwa Rais ni kazi muhimu ya maana na ya thamani na tusitamani nyengine,” amesema

Profesa Kabudi amesema, “ukipewa wajibu huo ni mkubwa, uheshimu, ufanyie kazi, ridhika nao, sio kwa maana yoyote ile, ukijua daraja na daraja jingine liache  na hasa unapopewa kazi na mkuu wa nchi.”

Amesema, kasinya Rais Magufuli ya kutaka kuleta maendeleo inatokana dhamira ya kutekeleza ndoto na mipango ya Mwalimu Nyerere.

Amesema nchi inakwenda kutimiza miaka 60 tangu kuwa huru kwa kishindo cha kufanikisha mambo makubwa ndani ya miaka mitano.

error: Content is protected !!