September 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Profesa Kabudi ‘ajitosa’ kugombea ubunge Kilosa

Prof. Palamagamba Kabudi, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki

Spread the love

PROFESA Palamagamba Kabudi, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, ameonyesha nia ya kutaka kugombea ubunge jimbo la Kilosa mkoani Morogoro, katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2020. Anaripoti Mwandishi Wetu, Kilosa … (endelea).

Kabudi ameonyesha nia hiyo leo tarehe 29 Juni 2020 wilayani Kilosa, wakati akihutubia katika hafla ya uwekaji jiwe la msingi ujenzi wa mahandaki manne yenye urefu wa kilomita 2.7 ya reli ya kisasa kutoka Morogoro hadi Makutupora.

Licha ya kwamba hakutaja hadharani nia ya kugombea ubunge Kilosa, Profesa Kabudi amesema, kama atapata kibali kutoka kwa Mungu, hatakataa kuwa mtumishi wa wananchi wa Kilosa.

Profesa Kabudi ametoa kauli hiyo wakati anawahimiza wananchi wa Kilosa, kumpa nafasi nyingine Rais John Magufuli, ya kuliongoza Taifa la Tanzania katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2020.

“Kilosa haikuwa hapa na haistahili kuwa hapa, itumieni nafasi hii aliyotupa Mungu vizuri, kwa kutupa rais mwenye maono.”

“Kwa nini hatufanyi hivyo? Tubadilike na tunakiongozi mwenye maono na mimi mtoto wenu ikimpendeza Mungu na nikipata kibali na taratibu, sikatai kuwa mtumishi wenu,” amesema Profesa Kabudi huku akishangiliwa na mamia ya watu waliokuwepo.

Soma zaidi:-

Akizungumza katika mkutano huo, Profesa Kabudi amesema, wilaya ya Kilosa haikustahili kubaki nyuma katika maendeleo, kwa kuwa ni wilaya yenye rasilimali nyingi, ambazo kama zitatumika vizuri, zitachagiza maendeleo ya mkoa huo.

Hata hivyo, Profesa Kabudi amemshukuru Rais Magufuli kwa kuikumbuka wilaya hiyo kwa kupeleka barabara na miradi ya maji.

“Namshukuru Rais Magufuli kwa kuirudisha Kilosa kwenye heshima yake ya zamani, wote mnafahamu kote huko kunahitaji maendeleo,” amesema Rais Magufuli.

Jimbo ambalo Profesa Kabudi anakusudia kugombea kwa sasa mbunge anayemaliza muda wake ni wa CCM, Mbaraka Bawazir.

error: Content is protected !!