Tuesday , 23 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Profesa Assad: Niliondolewa CAG bila utaratibu
Habari za SiasaTangulizi

Profesa Assad: Niliondolewa CAG bila utaratibu

Prof. Mussa Assad alipohojiwa na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maadili, Haki na Madaraka ya Bunge
Spread the love

 

PROFESA Mussa Assad, aliyewahi kuwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali ya Tanzania (CAG) amesema, aliondolewa katika wadhifa wa U CAG kwa sababu waliopaswa kusimamia Katiba hawakufanya hivyo. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Amesema, Ibara ya 144 ya Katiba ya Tanzania, inayozungumzia jinsi ya kumwondoa madarakani CAG hayakufuatwa.

Profesa Assad amesema hayo leo Jumatano, tarehe 6 Oktoba 2021 jijini Dodoma katika mdahalo wa kuchambua Kitabu cha Rai ya Jenerali Ulimwengu na masuala ya Katiba, ulioandaliwa na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC).

Alipopewa wasaa wa kutoa neno la awali, Profesa Assad amesema, leo Jumatano ndiyo ametimiza miaka 60 tangu alipozaliwa na ni umri ambao ungemwezesha kumaliza muda wake wa U CAG lakini yeye aliondolewa kabla ya muda.

           Soma zaidi:-

“Mara nyingi, ikitajwa CAG aliyemaliza muda wake huwa siipendi sana kwani mimi nilipotolewa ofisini sikuwa nimemaliza muda wangu.”

“…na kwa kweli binafsi ni jambo linaloniudhi na linanifanya kusema hatukuwa wazuri katika kusimamia katiba yetu na tumeachia mambo yamekwenda hovyo hovyo,” amesema Profesa Assad.

“Mimi ni CAG niliyemaliza muda wangu, hapa ndipo kuna umuhimu wa Katiba na si umuhimu tu bali umuhimu wa kusimamia Katiba. CAG anayeweza kumaliza muda wake akiwa ametimiza miaka 60, mimi niliondolewa nikiwa bado,” amesisitiza.

Aliyekuwa kuwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali ya Tanzania (CAG), Profesa Mussa Assad

Profesa Assad aliyekuwa ameingia kwenye mgogoro na Bunge la Tanzania, alijikuta akiwekwa kando tarehe 3 Novemba 2019 baada ya aliyekuwa Rais wa Taifa hilo, Hayati John Pombe Magufuli, kumteua Charles Kichere kuchukua wadhifa wake.

Kabla ya uteuzi huo, Kichere alikuwa Katibu Tawala Mkoa wa Njombe (RAS).

Mvutano baina ya CAG na Bunge ulitokana na moja ya mahojiano aliyoyafanya na chombo kimoja cha habari nje ya Tanzania Desemba 2018 kuzungumzia udhaifu wa muhimili huo katika kuchukua uamuzi kwa baadhi ya mapendekezo wanayoyatoa kwenye ripoti za kila mwaka.

Kauli hiyo ilionekana kutopendezwa na Bunge ambapo Spika wa Bunge, Job Ndugai alimtaka kufuta kauli hiyo na haikuwa hivyo na kuagiza Profesa Assad kuhojiwa na kamati ya maadili ya Bunge kwa kudharau Bunge.

Profesa Assad alihojiwa na kamati hiyo Januari 2019 na miezi mitatu baadaye yaani Aprili 2019, taarifa ya kamati hiyo iliwasilishwa Bungeni na wabunge kuijadili kisha kuazimia kutokufanya kazi na yeye.

”Tatizo letu ni maneno ambayo Profesa Musa Juma Assad aliyasema kule Marekani na majuzi alipowaita waandishi wa habari Dodoma akarudia tena kuwa ataendelea kuyasema maneno hayo,” alisema Spika Ndugai wakati huo akizungumzia suala hilo

aliongeza “maneno yale sisi tumeyakataa kuwa si maneno ya kistaarabu hilo ndio tatizo, na sio taarifa iliyotolewa.’ Huku akisisitiza wao watafanya kazi na Ofisi ya CAG na si CAG Profesa Assad.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

Mpwa wa Magufuli mbaroni kwa kusambaza picha za utupu

Spread the loveJESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewakamata...

Habari za Siasa

Serikali kuanzisha mradi wa Gridi ya maji ya Taifa

Spread the loveWaziri wa Maji, Jumaa Aweso amesema katika mwaka wa fedha...

Habari za Siasa

Rais Samia aridhishwa utendaji mabalozi, awapa neno

Spread the loveRais wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan amewapongeza mabalozi  wanaowakilisha ...

error: Content is protected !!