Wednesday , 17 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Profesa Assad awananga viongozi ‘mazuzu’
Habari za Siasa

Profesa Assad awananga viongozi ‘mazuzu’

Aliyekuwa Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Prof. Mussa Assad
Spread the love

 

PROFESA Mussa Assad, aliyewahi kuwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali ya Tanzania (CAG) amekerwa na viongozi wenye uwezo wa kuzungumza ukweli kwa maslahi ya Taifa kushindwa kufanya hivyo. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

CAG huyo wa zamani amesema hayo leo Jumatano, tarehe 6 Oktoba 2021 jijini Dodoma, akizungumza katika mdahalo wa kuchambua Kitabu cha Rai ya Jenerali Ulimwengu na masuala ya Katiba, ulioandaliwa na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC).

Katika mdahalo huo, Profesa Assad amempongeza Jenerali Ulimwengu kwa ujasiri wake wa kuandika na kuzungumza kile anachokiamini pasina woga wowote.

            Soma zaidi:-

“Nimekuwa msomami mzuri wa makala za Jenerali Ulimwengu na ni mtu tunaye mtazama kama hazina, kama kuna jambo la kusema atalisema, kwani kwa sasa kuna watu wamekuwa kama mazuzu.”

“Mtu amesoma sawasawa, anamwogopa mtu mwingine kwa sababu tu anatumia V8, nyumba ya serikali, anaogopa nikitoka hapa nitapata riziki wapi, mbona mimi nina miaka miwili nimeondolewa ofisini maisha yanaendelea,” Profesa Assad

Leo Jumatano, Profesa Mussa ametimiza miaka 60 tangu alipozaliwa ambapo washiriki wa mdahalo huo, wamemwimbia wimbo maalum wa ‘Happy Birthday.’

“Tunaishi siku moja, maisha yetu ni mafupi sana. Kila kunapokucha hakikisha unafanya vizuri sana kwani hakuna anayeijua kesho,” amesema Profesa Mussa

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Samia arejesha mikopo ya 10%, bilioni 227.96 zatengwa

Spread the loveRAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amerejesha utaratibu wa utoaji mikopo...

Habari za Siasa

Rais Samia amfariji mjane wa Musa Abdulrahman

Spread the loveRais Samia Suluhu Hassan leo Jumanne amempa pole Mwanakheri Mussa...

Habari za Siasa

Nape: Wanasiasa, wanahabari, wafanyabiashara mteteeni Samia

Spread the loveWaziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari na Mawasiliano,...

Habari za Siasa

CAG: TAWA imegawa vibali vya uwindaji bila idhini ya waziri

Spread the loveRIPOTI ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali...

error: Content is protected !!